‘Nyufa’ zajitokeza Bunge la Afrika Mashariki;
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki,
(EALA), wameingia katika mpasuko, kutokana na baadhi ya wabunge hao
kupinga kutumia ukumbi wa kisasa wa Bunge hilo uliopo Arusha kwa vikao
vyote, na badala yake baadhi wanataka kuendelea na utaratibu wa kufanya
vikao vya Bunge katika kila nchi wanachama.
P.T
Habari za uhakika toka ndani ya
Wabunge wa Afrika ya Mashariki, walioanza kikao cha Bunge la jumuiya
hiyo juzi jijini hapa, zimebainisha kuwa, licha ya Kamati ya Uongozi wa
Bunge hilo, kufikia uamuzi ya vikao vyote sasa kufanyika Arusha, lakini
bado kuna wabunge wanapinga.
Kikao cha kamati ya uongozi
kilichoongozwa na mwenyekiti wake ni Spika wa Bunge hilo, Dk Magreth
Zziwa, kiliamua baada ya kukamilika jengo la Bunge, likiwa na ofisi kwa
kila mbunge sasa vikao vyote vifanyike Arusha ili pia kupunguza gharama.
Awali Bunge hilo, katika vikao vyake
vya Arusha, vilikuwa vikifanyika katika Jengo la Kituo cha Mikutano cha
Arusha (AICC) kwa kukodi.
Katika hatua ya kuonyesha kushawishi
wabunge kuanza kutumia jengo lao jipya kwa mikutano yote, Mbunge wa
Bunge hilo wa Tanzania, ShyRose Bhanji aliipongeza Serikali ya Tanzania
kwa kutoa ardhi bure kwa ujenzi wa jengo la EAC lenye ukumbi wa kisasa
wa Bunge.
Ofisa Habari za Bunge la Afrika ya
Mashariki, Bobi Odiko, jana alikiri kuwapo mjadala wa kutaka kuendelea
kuhamisha vikao vya Bunge au sasa kufanyika Arusha huku akisema anaamini
wataafikiana.
"Ni kweli mijadala inaendelea na leo (jana) kulikuwa na kikao juu ya suala hili lakini naamani mwafaka utafikiwa"alisema Odiko
No comments:
Post a Comment