EU YAKEMEA MAUAJI YALIYOFANYIKA MISRI
Muungano wa Ulaya umeonya Misri kuwa
itarejelea uhusiano wake na nchi hiyo katika siku chache zijazo. Katika
taarifa , Muungano huo umesema kuwa wito wa kuheshimiwa demokrasia na
haki za kimsingi za binadamu haziwezi kuruhusiwa kuendelea kuvunjwa.
P.T
P.T
EU pia imeelezea wasiwasi wa
kuongezeka umwagikaji wa damu. Umeongeza kuwa mauaji yaliyofanywa
hayawezi kuelezewa wala kukubaliwa. EU imeahidi mabilioni ya dola kama
mkopo na msaada kwa Misri kwa mwaka uliopita na mwaka ujao.
Mustakbal wa serikali
Baraza la mawaziri nchini Misri
limeitisha mkutano wa dharura wakati ambapo mzozo wa kisiasa nchini humo
kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo
Mohammed Morsi umesababisha raia wengi kupoteza maisha yao.
Kaimu waziri mkuu Hazem El Beblawi
amependekeza kuvunjiliwa mbali kwa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo
bwana Morsi ni mwanachama .
Siku ya Jumamosi, polisi
wakishirikiana na wanajeshi walifanikiwa kuwaondoa wafuasi wa vuguvugu
hilo katika msikiti wa Al-Fateh mjini Cairo ambapo maelfu ya
waandamanaji walikuwa wamekita kambi.
Vikosi vya usalama vimesema
viliwakamata maelfu ya raia wakiwemo baadhi ya viongozi wa vugu vugu la
Muslim Brotherhood na kwamba takriban watu 250 wanachunguzwa kwa
mashtaka ya mauaji na ugaidi
No comments:
Post a Comment