KIJANA ALIYEKAMATWA NA MWAKYEMBE
Siku moja baada ya ziara ya kushtukiza
ya waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe, kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-Salaam, kiasi kikubwa cha dawa
za kulevya kimekamatwa uwanjani hapo katika harakati za kusafirishwa
kwenda nchi za nje.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard
Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za
madawa ya kulevya aina ya heroine
Juhudi za Dk. Mwakyembe na Dawa za Kulevya, Amnasa Rasta Akisafirisha Madawa Uwanja wa JNIA Dar es Salaam
JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana
zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na
dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia
hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita
yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana
na madawa hayo ya kulevya.
Akizungumza na vyombo vya habari leo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana
aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo)
ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka
kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi
lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na
mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo
kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu
kusafiri nayo kwa ndege.
Alisema kijana huyo kwa sasa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa
mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa
kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana
navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo
mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua
taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha
anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za
kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema
maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa
kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri
waliyoifanya.
"Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu
ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa
ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu
sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo...," alisema.
"Picha yake itasambazwa kila
sehemu...sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na
dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya
akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira
ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa
kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila
atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo
mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa
ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia
Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo
haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya
ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja
vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu,
jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es
Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu
yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka
yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na
kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya
kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi
karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja
wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong
Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao
yatawekwa hadharani muda wowote.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment