CCM YAMFUTA UANACHAMA NDUGU MANSOOR YUSSUF HIMID
Kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo
pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la
kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi wa Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-
hd
1. Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2. Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3. Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya
kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid,
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu
ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo
wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa
sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
No comments:
Post a Comment