EZEKIEL KEMBOI ANYAKUWA MUDALI YA DHAHABU
Ezekiel Kemboi ameshinda ubingwa wake
wa tatu wa dunia wa mbio za meta 3000 kuruka maji na viunzi katika
mashindano ya ubingwa wa dunia wa riadha mjini Moscow.
P.T
Bingwa huyo mara mbili wa Olympiki
mwenye umri wa mika 31 alikimbia mbio hizo kwa muda wa dakika 8 na
sekunde 06.01 kunyakua medali ya dhahabu ,huku mkenya mwenzake Conseslus
Kipruto mwenye umri wa 18 akishinda medali ya fedha kwa kukimbia mbio
hizo kwa dakika 8 na sekunde 06.37 na Mahiedine Mekhissi Benabbad wa
Ufaransa alipata medali ya shaba kwa dakika 8 na sekunde 07.86 na
kuipokonya Kenya fursa ya kusomba medali zote kwa kumpiku Paul Kipsiele
Koech.
Wakenya wanne katika fainali hiyo ndio waliyoongoza mbio hizo kuanzia mwanzo.
Benabbad alionekana kutishia kuwapita lakini Kemboi aliongeza kasi na kuthibitisha kua ni mwanariadha hodari kutoka Kenya katika miaka ya hivi karibuni.
Kemboi ameifikia rekodi ya Mkenya mwenzake Moses Kiptanui ya kushinda ubingwa wa dunia mara tatu mfululizo katika ya miaka 1991-1995.

No comments:
Post a Comment