TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, August 23, 2013

NAIBU WAZIRI KATIBA NA SHERIA ATOA MSAA WA BAISKELI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU

Mheshimiwa Angel Kairuki akiwa na watoto wake Kemy na Esta walopokuwa wamekuja kukabidhi msaada huo wa Baiskeli kwa watoto hao

Mhesimiwa akiwa anaongea na Mtoto Halima huku akiwa amemkalisha katika kiti cha baiskeli yake
Wazazi wakiwa na watoto wao baada ya kukabidhiwa baiskeli zao



Mtoto wa Waziri akiwa namuendesha mmoja wa watoto wenye ulemavu

Mheshimiwa Angel anatakiwa awe mfano wa kuiga kwa kuishirikisha familia yake katika kushiriki kazi za kijamii ili hapo baadae na wao waweze kutenda matendo mema kama hayo kwa kuwajali wenye shija katika jamii itakayowazunguka Mungu aibariki familia yako.

Mheshimiwa akiwa anamuendesha mtoto ni njia ya kuonesha ni jinsi gani anawajali na kuwapenda watoto





Mheshimiwa akikabidhi  baadhi ya zawadi zingine kwa mzazi kwa niaba ya watoto


Mtoto akifurahia zawadi zake



NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki ametoa msaada wa
maalum wa baiskeli 30 kwa watoto wenye ulemavu kupitia shirikisho la Vyama
vya Watu Wenye Ulemavu nchini (SHIVYAWATA).
 
Angellah alikabidhi viti hivyo jana, vyenye thamani ya zaidi ya sh.
milioni 12, kwa baadhi ya watoto hao 10 waliofika kwenye makabidhiano , na baadaye kuwafikia watoto wengine wenye mahitaji.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi, alisema viti hivyo ni maalum kwa
watoto wenye miaka kuanzia sifuri hadi tisa, na ametoa kutokana na
kuguswa na matatizo ya wenye ulemavu na pale anapopata nafasi
anawakumbuka.
 
"Nimekuwa nikifanya kazi zaidi na watoto wenye ulemavu wa kusikia
(Viziwi), lakini pia nikaona kuna kundi lina mahitaji zaidi, hivyo kwa
kidogo nilichopata  nikawambuka, nafanya kazi kwa kushirikisha familia
yangu,  sitaishia hapa nitawasaidia zaidi kwa kadri
nitakavyojaaliwa,"aliongeza kiongozi huyo aliyekuwa ameambatana na
wanaye wawili.
 
Akishukuru kwa msaada huo, Katibu wa SHIVYAWATA, Felician Mkudem
alisema kuwa  wanafarijika sana kuona watu muhimu kama Angellah,
wanakumbuka na kuwajali.
 
"Kiongozi wa serikali ndiye jicho na sauti za watu wenye ulemavu,
hivyo kwa kutusaidia vifaa saidizi kwa wtaoto wenye ulemavu ni faraja
kubwa sana, kwani mambo hayo ni miongoni mwa tunayoyapigania,"alisema.
 
Mkude alitumia fursa hiyi kukamabidhi nyaraka mbalimbali, ikiwemo
mpango mkakati wa ukondaishaji wa watu wenye ulemavu na sheria
mbalimbali zinazowahusu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Viungo, (CHAWATA), Shida
Salum aliishukuru serikali ya Rais Kikwete kuwakumbuka watu wenye
ulemavu na kuwafanyia mengi kwa ajili ya ustawi wao.
 
Wazazi wa watoto hao walishukuru kwa msaada huo na kwamba utawasaidia
watoto wanaosoma waliokuwa wanabebwa kwenda na kurudi shule, na
wengine waliokuwa hawajaanza masomo kutokana na hali ngumu ya
kuwafikisha shuleni.
 
 
mwisho.

No comments:

Post a Comment