ISRAEL YAJENGA MAKAZI ZAIDI YA WALOWEZI
Serikali
ya Israel imeidhinisha ujenzi wa nyumba mpya zaidi ya 1,000 katika
makaazi ya Wayahudi kwenye maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Israel.
Nyumba za Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina
Nyumba za Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina
Waziri wa Makaazi wa Israel, Uri
Ariel, alisema nyumba hizo zitajengwa Ufukwe wa Magharibi na masahriki
mwa Jerusalem ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Israel.
Tangazo hilo limetolewa siku tatu kabla ya mazungumzo ya amani baina ya Israel na Wapalestina kuanza tena mjini Jerusalem. (HM)
Waziri wa Makaazi wa Israel ametoa
idhini ya mwisho kujenga karibu fleti 1,200 katika maeneo yenye makaazi
ya Wayahudi, siku tatu tu kabla ya mazungumzo ya amani kati ya Israeli
na Palestinian kuanza tena.
Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas,
alishikilia kwa muda mrefu kwamba hatarejea kwenye mazungumzo bila ya
Israel kusitisha kujenga makaazi mepya kwenye maeneo inayoyakalia.
Lakini hatimaye alikubali kushiriki
katika mzungumzo baada ya Israel kusema kuwa itawaachilia huru wafungwa
wengi wa Kipalestina.
Makaazi ya Wayahudi katika Ufukwe wa Magharibi ndio swala kubwa linalokwamisha mazungumzo.
Makaazi hayo yanaonekana kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa, ingawa Israel inapinga hilo.Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment