TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, September 30, 2013

Jumuiya ya waKenya DMV waomboleza mauwaji ya Westgate 

Jumuiya ya waKenya DMV waomboleza mauwaji ya Westgate, Siku nane tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua zaidi ya watu 67 na kujeruhi wasiopungua 175.
_DSC5346_7fca4.png
MC Humphrey OneMic Muturi akiwa Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya kuomboleza mauwaji ya Westgate.
994603_532097310209374_2094062797_n_32cbc.jpg
Wakenya kutoka sehemu mbalimbali duniani wameungana na wenzao katika maombi na ishara za matumaini kwa wenzao wa nchini Kenya.(P.T)
65036_532087836876988_1409503866_n_c6352.jpg
Baadhi ya waKenya kutoka sehemu mbalimbali hapa DMV Siku ya Jumapili Sept 29 walikutana Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C kwa maombolezo ya mauwaji yaliotokea jijini Nairobi siku ya Jumamosi Sept 29 ndani ya Westgate Mall jijini Nairobi Kenya.
1381567_532092906876481_1434818568_n_9821a.jpg
Pastor Maurice Kinyanjui akifungua hafla hiyo kwa dua maalumu ya maobolezo ya mauwaji ya Westgate yaliofanyika Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C
1381214_532096473542791_1210482955_n_4aa54.jpg
Jumuiya ya waKenya na rafiki wa wanajumuia hao walikutana Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya kuwakumbuka, kuwaombea na kuwapa matumaini wenzao walioathirika na tukio hilo.
9411_532107810208324_616912281_n_61c92.jpg
Walianza kwa ufunguzi kuwaombea dua walioathirika na tukeo hilo lilitokea Siku ya Jumamosi Sept 21, ambapo kundi la Al shabab walivamia na kuteka eneo la sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate Mall Jijini Nairobi Kenya
1383089_532106933541745_694309079_n_8b653.jpg
Waliendelea kwa kukumbushana mengi yakiwemo kusisitiza kwa upendo wa kua kitu kimoja bila ya kujali tafauti zao na kuvumilia kwa yote yaliotokea kwani Kenya ni nchi ya amani.
Siku nane tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua zaidi ya watu 67 na kujeruhi wasiopungua 175.
1240111_532107156875056_1825582902_n_d4800.jpg1383971_532107323541706_1719921663_n_0aaa4.jpg

Dk SHEIN AMPONGEZA RAIS WA CHINA

sheinpx_214d8.jpg
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa China, Xi Jinping kwa kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Katika salamu zake hizo, Rais wa Zanzibar amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa China katika kusherehekea miaka 64 ya uhuru wa nchi hiyo pamoja na urafiki na mshikamano uliodumu kwa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili.(P.T)
Dk Shein ameitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya China kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika sekta zote za maendeleo chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti.
Ameelezea matumaini yake kuwa ushirikiano baina ya Serikali ya China na Wananchi wa Zanzibar utaendelea kuimarika zaidi.

HAMAD :KIKWETE USISAINI MUSWADA

seif_1e39b.jpg
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad amesema mgogoro wa Muungano uliopo unatokana na kufichwa kwa makubaliano yaliyowekwa na waasisi wa Muungano na kusema kero hizo hazitakwisha hadi kutakapoundwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba.
Alisema hayo juzi wakati wa kongamano la Wazanzibar waishio Bara na kusema Muungano uliotiwa saini na waasisi wa Muungano huo umefichwa na kusema dawa yake ni Serikali tatu na Muungano wa mkataba.(P.T)
Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013 kwa maelezo kuwa una kasoro.
"Wazanzibari wenzangu na mimi pia ni mmoja wao ambao tunataka Muungano wa mkataba, nilipoulizwa na tume nilisema nataka Muungano wa mkataba nadhani nanyi pia mawazo yenu ni kama mimi," alisema Hamad.
Hamad aliisifu Serikali ya Kikwete kwa kuwaachia wananchi wenyewe kuiandika katiba yao na kumwomba asikubali kutia saini muswada huo wa sheria.
Alisema Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kama ilivyo kwa nchi nyingine hivyo inahitaji kurejeshewa mamlaka yake na kuwa na uamuzi ikiwa na pamoja kurejeshewa kiti chake katika Baraza la Umoja wa Kimataifa.
"Zanzibar iko na haki ya kuingia mikataba na jumuiya za kimataifa kama ilivyo nchi nyingine, tunataka dola ya Zanzibar iliyo nchi kamili kama ilivyokuwa zamani, Muungano umeifuta Zanzibar katika ramani ya kimataifa," alisema na kuongeza:
"Hivi sasa Zanzibar haina haki ya kusema inajiunga na jumuiya yoyote ya kimataifa, kikwazo hiki ni kufichika kwa makubaliano ya Muungano kutoka kwa waasisi wetu."

SUAREZ AFUNGA 2 LIVERPOOL IKIIUA SUNDERLAND 3-1 

suarez debd5
Luis Suarez akishangilia kwa kuonyesha picha ya mkewe na binti yake na mtoto wake mpya wa kiume, Benjamin (HM)

suarez2 9aaee
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amerejea na moto katika Ligi Kuu ya England baada ya kumaliza adhabu yake ya mechi 10, leo akifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 wa Liverpool dhidi ya Sunderland.
Ntyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 36 na 89 wakati lingine lilifungwa na mshambuliaji pacha wake, Daniel Sturridge dakika ya 28 na kufutia machozi la wenyeji lifungwa na Emanuele Giaccherini dakika ya 52.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Henderson, Gerrard, Lucas, Jose Enrique, Moses/Sterling dk75, Sturridge na Suarez.
Sunderland: Westwood, Gardner, O'Shea, Cuellar, Colback, Larsson/Mavrias dk85, Cattermole/Celustka dk74, Ki,Johnson, Altidore na Giaccherini.

WIZARA YA AFYA YAICHAPA 3-0 WAKALA WA JIOLOJIA 

dom 671df
Timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii yawa mbogo kwenye michezo ya Shimiwi katika mechi zake zote kwenye mashindano yanayoendelea mkoani hapa. (HM)


Katika mechi ya leo asubuhi ya raundi ya pili ya mtoano iliyochezwa kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma(UDOM), Afya imewachabanga magoli matatu wenyeji timu ya wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) ya mkoani hapa na hivyo kufanikiwa kuingia raundi ya tatu ya mtoano itakayoanza mapema kesho.


Afya iliweza kuona nyavu za GST katika dakika ya kumi ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo, ambapo goli la kwanza lilifungwa na mchezaji mwenye jezi namba 10 mgongoni Patrick Mangungulu.


Kipindi cha pili dakika ya tatu Afya ilifanikiwa kuziona tena nyavu za wapinzani hao, goli lililofungwa na Christopher Nandadya aliyepewa pasi nzuri na mshambuliaji Emmanuel Zunda.


Katika kipindi cha lala salama mchezaji wa afya dkt. Iddy Ramadhani alipokea pasi nzuri toka kwa Japhari Ngalipa na hivyo kusababisha kumaliza mchezo huo kwa kifua mbele.


Katika raundi ya kwanza ya ligi, Afya iliibamiza RAS Singida kwa mabao 7 kwa Sifuri na mechi ya pili walifanikiwa kuwazamisha RAS Kilimanjaro kwa mikwaju minne kwa moja.


Hatahivyo katika mechi ya tatu RASMorogoro waliwaotea Afya na hivyo kufanikiwa kuifunga bao moja kwa sifuri. Chanzo: Catherine Sungura (MOHSW)
Dodoma

MANCINI ATUA UTURUKI KUSAINI MKATABA WA KUINOA GALATASARAY 

 mancin2 49684

Roberto Mancini amekwenda Uturuki kwa ajili ya kusaini kuifundisha Galatasaray (HM)
mancin ce341
KOCHA Roberto Mancini jana amekwenda mjini Istanbul, Uturukikufanya mazungumzo ya kusaini Mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Galatasaray utakaokuwa na thamani ya Pauni Milioni 4.6 kwa mwaka.
Mancini, amekuwa 'juu ya mawe' tangu atupiwe virago Manchester City mwishoni mwa msimu na anatarajiwa kutambulishwa kurithi mikoba ya Fatih Terim Jumanne.
Mabingwa hao wa Uturuki pia wamekubali kumlipa Mtaliano huyo bonasi ya Pauni Milioni 5.86 kama watavuka hatua waliyofika mwaka jana Ligi ya Mabingwa na kufanikiwa kuingia Robo Fainali.
Mancini anatarajiwa kukutana na Rais wa klabu, Unal Aysal Jumatatu kufikia makubaliano ya mwisho ya Mkataba, kwa mujibu wa wakala Muzzi Ozcan ambaye alifanikisha kuziunganisha pande hizo mbili, baada ya klabu hiyo kumfukuza Terim. Chanzo: binzubeiry

MISS UTALII KUTANGAZA KUPATIKANA NYATI WA AJABU NGORONGORO 

NYATI-MWEUPE-NGORONGORO1 700ec
Nyati mweupe nayepatikana Ngorongoro (HM)
MISS-TOURISM-TZZ1 a93f9
Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.
Ngorongoro Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania, nahazina ya Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu zote, ili iweze kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa, lakini pia kukuza na kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya. Naupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao za kukuza utalii na kupambana na majangili , nawaomba kuimarisha na kuongeza mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine wala nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi la mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la nyati wengine kandokando ya barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo liliwavutia na dereva wa basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa wafanyakazi hao kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na kamera walizokuwa nazo.
Hadija ameushukuru uongozi wa Ngorongoro , kwa kumpatia DVD zaidi ya 100 ya hifadhi hiyo,ambazo atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo vya Televisheni vya nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya Dunia ya Miss Tourism World 2013 mwaka huu. Baada ya kurudi nitazunguka nchi nzima na dunia nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Miss Tourism Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Chanzo: fullshangweblog

UKOSEFU WA ELIMU WASABABISHA UJINGA, MARADHI NA UMASKINI 

salma fa5c4
Watoto wengi katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na tatizo la ujinga, maradhi na umaskini hivyo basi kupatikana kwa elimu bora kutawasaidia kujikwamua na matatizo hayo pindi watakapomaliza masomo yao na kupata ajira na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha. (HM)

Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na walimu walioshiriki katika warsha ya elimu iliyoandaliwa na Taasisi ya Malaika na kufanyika katika chuo kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln .
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema jamii nyingi inajitahidi kupambana na matatizo yanayozakabili watoto wao lakini kama kutakuwa na ushirikiano wa pamoja itasaidia matatizo hayo kutatulika kirahisi.
"Warsha hii inaonyesha kuwa Dunia ni moja, ni kama kijiji bila ya kuangalia mipaka iliyopo , kutokana na hili tunatakiwa kutumia utaalamu wetu katika kushirikiana kwa pamoja ili kutatua matatizo yanayotukabili na kutumia pamoja rasilimali zilizopo", alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Malaika Dk. Natalie Hahn alimshukuru Mama Kikwete kwa kukubali kushiriki katika warsha hiyo kwa kuwa ni wanawake wachache kama yeye wanaoweza kuwa karibu na jamii inayowazunguka.
Alisema kuwa elimu ni nyenzo muhimu katika maisha mtu akiwa na elimu anaweza kwenda popote pale apatakapo kutokana na hilo ndiyo maana anachangisha vitabu kwa ajili ya wanafunzi katika mabara yote ili nao waweze kupata elimu kama aliyoipata yeye.
"Walimu mnatakiwa kuwa wa kimataifa ili muweze kufundisha na wengine wajivune na kutaka kuwa kama nyinyi, mtafute wafadhili wa masomo yenu ili muweze kusoma zaidi pia muwasaidie watoto ambao wanahitaji kusaidiwa kwani kama mtoto akikosa ada au nguo za shule Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia watoto (UNICEF) linawasaidia watoto wa aina hii", alisema Dk. Natalie.
Aliwataka walimu walioshiriki katika kongamano hilo wajitahidi kuwa na shule dada nchini Tanzania na kujenga mahusiano nao ili waende kufundisha kule watajifunza mambo ambayo ni tofauti, watumie rasilimali walizonazo kuwasaidia wanafunzi ili nao wawakufundishe wengine.
Katika warsha hiyo Mama Kikwete alikabidhiwa hati ya ukazi wa jimbo la Nebrasca na Dk. Marjorie Kastelnin ambaye ni mlezi wa wanafunzi katika kitivo cha Elimu na Sayansi ya Jamii.
Mama Kikwete pia alikutana na Mke wa Gavana wa jimbo hilo Mama Sally Ganem ambaye alimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya nchini Tanzania ya kuwasaidia kina mama na watoto wa kike kupata elimu.
"Kazi unayoifanya ni kubwa kwani inagusa maisha ya watu, elimu ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya binadamu mtu bila ya kuwa na elimu hawezi kufanya kitu chochote wewe unawasaidia watoto wa kike kupata elimu na kuwaandalia maisha yao ya baadaye, nakupongeza sana kwa hilo", alisema Mama Ganem.
Alisema kuwa fani yake yeye ni mwalimu kutokana na majukumu aliyonayo hafundishi kwa sasa, lakini kwa kuwa anawapenda watoto ameanzisha program ya kutoa chakula cha asubuhi kwa wanafunzi wa shule za msingi jambo ambalo mme wake Gavana Dave Heineman amemuunga mkono kwa kutoa chakula cha mchana kwa watoto hao. Chanzo: Anna Nkinda

MKONGO WA TAIFA WAHUJUMIWA 

2545656_929f8.jpg
Waziri Prof. Mbarawa akiangalia waya wa mkongo uliokatwa
Imeandikwa na Pamela Mollel, via Jamii blog, Arusha — Mkongo wa Taifa unakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu hata kabla haujakamilika kujengwa kwa Nchi nzima kutokana na baadhi ya Wananchi kuhujumu Mkongo huo kwa kukata nyaya katika barabara kuu ya Arusha - Namanga hadi Nairobi.
Changamoto hiyo imeibuliwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na kuhujumiwa vibaya juzi Mkoni Arusha katika ziara yake ambapo amesema kitendo hicho kimeletea hasara Taifa. Waziri Mbarawa alisema kuwa wananchi wasio waaminifu wenye nia ya kujitajirisha hisivyo halali wamekuwa wakikata nyaya za Mkongo huo wakidhani kuwa kuna shaba ndani ya nyaya hizo.(P.T)
Pia Prof. Mbarawa alisema kuwa Wakala wa Barabara nchini,TANROADS wanawajibu wa kushirikiana na Shirika la Simu Tanzania, TTCL kabla hawaja kabidhi mradi wa ujenzi wa Barabara kwa Mkandarasi ili kuepuka kuharibu miundombinu hiyo yenye kuwaletea wananchi mawasiliano, "Kilichofanywa na mkandarasi wa barabara hii siyo sahihi kabisa wamekata nyaya na kuharibu miundombinu, kabla ya kuendelea na shughuli za barabara walipaswa kushirikiana na TTCL," alisema Waziri.
Watumiaji wa kubwa wa Mkongo huo wa Taifa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato, TRA ambapo kaimu Afisa Forodha wa kituo cha Namanga, Aminiel Italisa alisema kuwa mkongo huo utarahisisha kazi zao.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mkongo wa Taifa na mawasiliano Adin Mgendi alisema kuwa pamoja na mkongo huo kurahisisha mawasiliano hapa nchini na pia Tanzania inategemewa na nchi zilizo mbali na bahari ya Hindi ili kuziunganishwa na mkongo wa Kimataifa.
Alisema kuwa elimu inahitajika kwa wananchi ili kuelewa umuhimu wa mkongo wa Taifa jamba ambalo litapelekea mrdi huo kutohujumiwa Tanzania itatumia zaidi ya Dola za Kimarekani milioni mia mbili kukamilisha ujenzi wa mkongo huo wa mawasiliano.

ICC INAHARIBU MAHUSIANO YAKE NA AFRIKA - RAIS KIKWETE

zzzzzzzzzzzjk_f1554.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mwenendo wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuhusu Bara la Afrika na viongozi wake, unainyima Mahakama hiyo nafasi kubwa ya kuungwa mkono na Bara la Afrika.
Rais Kikwete pia amelaani vikali mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya vikosi vya kimataifa vya kulinda amani katika nchi mbali mbali duniani wakiwamo walinda amani wa Tanzania.(P.T)
Rais Kikwete alitoa msimamo huo wa Tanzania mwishoni mwa wiki wakati alipohutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa (UNGA) mwaka huu, kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.
Katika hotuba yake fupi na iliyowavutia wasikilizaji, Rais Kikwete alisema kuwa ni dhahiri kuanzishwa kwa ICC kutokana na Mkataba wa Rome kulikuwa ni hatua muhimu sana katika mfumo wa kimataifa wa kupambana na makosa ya jinai.
"Kwa hakika kuundwa kwa Mahakama hiyo kuliweka mfumo mzuri wa kuondokana na watu kutenda vitendo vya jinai na kuweza kuepukana na kuwajibika kwa vitendo hivyo na Mahakama hiyo ilianzishwa kwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Afrika.
"Hata hivyo, muongo mmoja tu baada ya kuanzishwa kwa Mahakama hiyo, ni dhahiri kuwa mvutano umezuka kati ya ICC na Bara la Afrika. Sasa Mahakama hiyo inaonekana kama taasisi isiyojali maoni na msimamo wa Afrika, kwa mambo ambayo kwa maoni yangu, ni hofu halali ya Waafrika," amesema Rais Kikwete na kuongeza:
"Bado Mahakama hiyo inaendelea kupuuza maombi ya mara kwa mara ya Umoja wa Afrika. Ni jambo la kutia huzuni kuwa maombi ya kubadilisha muda wa kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Naibu Rais William Ruto yalipuuzwa na hata hayakujibiwa kabisa."
Ameongeza Rais: "Tabia hii imekuwa ni hitilafu kubwa ambayo inaleta kikwazo kwa ICC kushindwa kutimiza wajibu wake wa kupambana na tabia ya watu wanaofanya makosa ya jinai kutokuchukuliwa hatua. Kwa hakika, kugangamara kwa ICC hata katika masuala yaliyo wazi, kumethibitika kuwa kunainyima Mahakama hiyo nafasi ya kuendelea kuungwa mkono Barani Afrika."
Rais Kikwete alisema pia kuwa Tanzania sasa imekuwa moja ya nchi ambazo zinashiriki zaidi katika shughuli za kimataifa za kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania ina zaidi ya walinda amani 2,500 katika Darfur, Sudan; Lebanon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kuwa ni nchi ya sita katika Afrika na ya 12 duniani kwa kutoa walinzi wa amani duniani.
"Kwa hakika tunaridhishwa na mchango wetu mdogo katika shughuli hii. Na tunajua kuwa wakati mwingine tunalipa gharama kubwa na maisha ya vijana wetu kwenye shughuli hizi kama ilivyotokea majuzi katika Darfur na DRC. Waliopoteza maisha yao ni mashujaa wa taifa letu ambao maisha yao hayakupotea bure."
Aliongeza Rais Kikwete: "Vifo vya walinda amani wetu ni ukumbusho wa kutosha wa hatari zinazowakabili walinda amani wote duniani. Ni jambo la kuudhi, kwamba vikundi vyenye silaha na waharibifu wa amani duniani wanaongeza mashambulizi hayo dhidi ya watumishi wa amani. Ni lazima tulaani mashambulizi haya kwa nguvu zetu zote kwa sababu hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha mashambulizi haya ya kinyama ambayo ni kosa la kimataifa la jinai chini ya Sheria za Kimataifa."
Alisisitiza: "Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo wajibu wake mkuu ni kulinda amani na usalama wa kimataifa lazima liwe mstari wa mbele katika kulaani vitendo hivyo vya kinyama na haraka tu vinapotokea."
Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi katika Marekani na Canada ameondoka New York usiku wa leo, Jumamosi, Septemba 28, 2013, kurejea nyumbani ambako atawasili Jumatatu mchana.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Saturday, September 28, 2013

BARAZA LA USALAMA LAIDHINISHA AZIMIO KUHUSU SYRIA

syria_UN_fb37a.jpg
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio jana Ijumaa(27.09.2013)ambalo linataka kuondolewa kabisa kwa silaha za sumu nchini Syria lakini halitishii kuchukuliwa hatia za kuiadhibu serikali ya rais Bashar al-Assad iwapo haitatekeleza.
Kura hiyo ambayo imepigwa kwa kauli moja na wajumbe wote 15 wa baraza la usalama imefikisha kilele wiki kadha za majadiliano ya kidiplomasia kati ya Urusi na Marekani. Ilikuwa katika msingi wa makubaliano kati ya nchi hizo mbili yaliyofikiwa mjini Geneva mapema mwezi huu kufuatia shambulio la gesi ya sarin Agosti 21 mwaka huu katika kitongoji kimoja cha mji wa Damascus ambapo mamia ya watu wameuwawa.(P.T)
Makubaliano ya Urusi na Marekani
Makubaliano kati ya Urusi na Marekani yameepusha hatua za kijeshi dhidi ya serikali ya Assad, ambapo serikali ya Marekani inaishutumu kwa shambulio la hapo Agosti. Serikali ya Syria na mshirika wake, Urusi , wanawalaumu waasi wanaopambana na serikali kwa shambulio hilo. Sehemu moja ya azimio hilo , lilielezewa na wanadiplomasia wa baraza hilo kuwa ni muhimu, linaidhinisha mpango kwa mpito wa kisiasa nchini Syria uliokubalika katika mkutano wa kimataifa mjini Geneva Juni mwaka 2012. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema baada ya kura hiyo kuwa mataifa makubwa yanamatumaini ya kufanya mkutano wa amani kwa ajili ya Syria katikati ya mwezi Novemba mjini Geneva.
Ameliambia baraza hilo kuwa mpango wa kuondoa silaha za sumu za Syria , "sio leseni ya kuuwa kwa silaha nyingine." "Wakati tukifikia hatua hii muhimu, hatupaswi kusahau kuwa maovu yaliyotendeka nchini Syria yanaendelea kwa mabomu na vifaru, maguruneti na bunduki," amesema. "Kuzuwia aina fulani ya silaha sio ruhusa ya nyingine." Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa kura hiyo inaonesha kuwa "Hatua zina matokeo yake."
"Lengo letu kuu lilikuwa kuondoa na kuzuwia uwezo wa silaha za sumu nchini Syria. Na uwezekano wa matumizi ya nguvu za jeshi ambazo rais Obama amesiwasilisha zingeweza kutimiza lengo hilo. Lakini leo hii azimio hili linatimiza hata zaidi, kupitia njia za amani, litaweza kutoa kwa mara ya kwanza kuondoa kabisa uwezo wa nchi hiyo wa silaha za sumu," amesema. Azimio hilo haliruhusu kuchukuliwa hatua za moja kwa moja za kuiadhibu kijeshi ama kwa vikwazo serikali ya Syria iwapo haitatekeleza. Kwa msisitizo wa Urusi, azimio hilo linaweka wazi uamuzi wa pili wa baraza hilo kuwa utahitajika kwa ajili hiyo.
Urusi yatoa masharti
Lakini waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa baraza la usalama litakuwa tayari kuchukua hatua iwapo kutakuwa na ukiukaji wa azimio hilo uliothibitishwa na upande wowote wa mzozo huo. "Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa tayari kuchukua hatua chini ya ibara ya 7 ya katiba ya umoja wa Mataifa, kwa uwazi kabisa," amesema. Kikwazo kikubwa katika azimio hilo kilikuwa upinzani wa Urusi katika kuliandika chini ya ibara hiyo ya 7 ya mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambao unalipa baraza hilo mamlaka ya kuchukua hatua kutokana na maamuzi yake kwa kuweka vikwazo ama nguvu za kijeshi.
Urusi imeweka wazi , hata hivyo kuwa haitaunga mkono matumizi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Assad , mnunuzi mkuu wa silaha za Urusi. Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa , Bashir Ja'afari, amesema Uturuki , Saudi Arabia, Ufaransa, Qatar na Marekani zinapaswa kukubaliana na azimio hilo na ziwajibishwe iwapo zitaendelea kuwapa misaada waasi, ambao wanashutumiwa na serikali ya Assad kuwa walitumia gesi hiyo ya sumu dhidi ya jeshi la nchi hiyo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

50 WAUAWA KWENYE GHASIA SUDAN

130927090205 sudan 512x288 d nocredit 831fd

Maafisa wa usalama nchini Sudan wamewaua watu 50 katika maandamano yaliyofanywa kwa siku kadhaa kupinga hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo.
Polisi waliwatupia gesi ya kutoa machozi waandamanaji zaidi siku ya Ijumaa. (hd)
Taarifa zinazohusianaSudan
Maafisa wanasema kuwa chini ya watu 29 wamefariki na kusema kuwa serikali ilikuwa haiwezi tena kumudu gharama ya ruzuku ya mafuta.
Waandamanaji wameikosoa serikali ya Rais Omar al-Bashir kwa hatua hii na kumtaka aondoke mamlakani.
Taasisi ya elimu ya maswala ya haki na amani pamoja na shirika la Amnesty International zimesema kuwa watu wamepata majeraha ya risasi kwenye vifua na vichwa kulingana na jamaa, madaktari na waandishi wa habari.
Kijana mwenye umri wa miaka 14 alikuwa miongoni mwa waathiriwa wengi waliokuwa kati ya umri wa miaka 19-26. Waliongeza kusema kuwa mamia ya watu wamezuiliwa.
"Kuwaua kwa kuwapiga risasi watu kwenye vifua na vichwani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na Sudan lazima isitishe ghasia hizi mara moja,'' alisema Lucy Freeman, Naibu mkurugenzi wa shirika la Amnesty International.
Duru za hospitalini zimeambia BBC kuwa takriban watu 60 wameuawa.
Maafis wa serikali ya Sudan bado hawajasema chochote kuhusu mauaji hayo lakini waziri wa habari Ahmed Belal Osman alisema kuwa idadi ya vifo ambayo ni juu zaidi ya watu 29 sio sawa.
Ghasia zilianza Jumatatu pale serikali ilipoondoa ruzuku kwa mafuta ili kupandisha ushuru. Hatua ya serikali kupunguza gharama ya matumizi ya pesa za umma, ilisababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kuwaathiri sana watu wa kipato cha chini

TPA YASHIRIKI SIKU YA BAHARI DUNIANI 

PIC_2_4218e.png
Naibu Waziriwa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akizungumza na Kaimu Mkuuwa Bandari ya Mwanza, Bw. Edwin Kasyupa (kushoto) wakati alipotembelea Banda la TPA katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North hivi karibuni.(P.T)
PIC_5_68862.png
 Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akizungumza na wadau(hawapopichani) wanaohusika na sekta ya usafirishaji majini wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
PIC_6_1fe33.png
Naibu Waziriwa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji majini wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
TPA yaadhimisha siku ya Siku ya Bahari Duniani
Na Focus Mauki
Afisa Mawasiliano-TPA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshiriki maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North.
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Bahari Duniani (IMO) linaadhimisha Siku ya Bahari Duniani, Septemba 26 kila mwaka.
Maadhimisho hayo hufanyika mara moja kila mwaka ambapo pamoja na mambo mengine Jumuiya ya Kimataifa ya Bahari ikiongozwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO), huyaadhimisha kwa kutathimini usimamiaji wa ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira baharini na katika maziwa.
Tanzania ikiwamo nchi nyingine wanachama wa IMO huadhimisha siku hii kwa kufanya maonyesho ya siku mbili ambayo huandaliwa na SUMATRA. Kwa mwaka huu maonyesho haya yamefanyika Septemba 25 na kufikia kilele chake Septemba 26 mwaka huu.
Pamoja na kuwa na maonyesho kwa umma, SUMATRA iliandaa kongamano lililofanyika Septemba 26 ambalo lililenga kuonyesha mchango wa Sekta ya Bahari na Bandari katika kukuza na kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.
Kaulimbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni, 'Maendeleo endelevu: Mchango wa IMO kupitia Agenda ya Rio +20'. Kwa mujibu wa SUMATRA kauli mbiu ya mwaka huu imechaguliwa kuonyesha mchango wa IMO kwa mwaka 2013 katika kubeba jukumu la kutekeleza makubaliano ya kimataifa juu ya kuleta maendeleo endelevu yaliyoafikiwa katika kikao kilichofanyika Juni 20 hadi 22, 2012, Rio de Janeiro, Brazil kijulikanacho kama 'Rio+20'.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Alhaj Ahmad Kilima amenukuliwa na vyombo vya habari akisema Umoja wa Mataifa umechukua hatua za kimaendeleo kwa kuweka malengo mengi ili kufikia maendeleo endelevu ambayo hayatoathiri uwezo wa dunia, mfumo asilia pamoja na kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili jamii.
Sekta ya bahari ina mchango mkubwa katika mihimili mitatu ya maendeleo endelevu ambayo ni uchumi, jamii na utunzaji wa mazingira ya bahari. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha Bandari zake kote nchini, ili imeweka mazingira na miundombinu ya kisasa itakayotoa mchango katika kufikia malengo yaliyopo kitaifa na kimataifa

JAMII YATAKIWA KUWASAIDIA WATOTO KUPATA ELIMU 

 salma d57ef

Ilielezwa kwamba ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake katika jamii hakutakuwa na mtoto atakayekosa elimu kwa ajili ya kutokuwa na ada, vitabu na nguo za shule pia hakutakuwa na watu watakaokufa kwa kukosa chakula na malazi. (HM)

Ili kuhakikisha hayo yote yanafanikiwa jitihada za pamoja zinahitajika kwa wadau wote wa maendeleo kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana ili waweze kutimiza malengo na mipango waliyojiwekea.
Hayo yasemwa jana na mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha mada kuhusu uvumilivu na uongozi wa wanawake wa Afrika katika kukabiliana na changamoto za kibinadamu kwenye mkutano maalum wa kujadili utekelezaji wa huduma za kibinadamu barani Afrika uliofanyika mjini New York nchini Marekani.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kupatikana kwa elimu bora kwa mtoto kutamwezesha kupata fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya bora, kuongezeka kwa kipato cha familia na hivyo kujikwamua na hali ya umaskini.
"Kitaaluma mimi ni mwalimu nafahamu changamoto zinazowakabili watoto na familia zao wakati wanajitahidi kupambana na ujinga, magonjwa na maisha ya umaskini kutokana na hali hii, mimi naona kuwapatia elimu ni njia moja wapo itakayowafanya waweze kuepukana na umaskini kwani mara wamalizapo masomo yao wataweza kupata ajira na hivyo kujitegeme", alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa WAMA aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo kuwa aliamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo kupitia kwake ameweza kuhakikisha watoto wa kike wanakwenda shule kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kusoma kwani mtoto wa kike akikaa shule muda mrefu ndivyo anavyoweza kuepukana na mimba za utotoni, vifo wakati wa kujifungua na hali ya umaskini.
Mama Kikwete alisema, "kutokana na hali hii tumejenga shule ya sekondari ya mfano ya WAMA-Nakayama iliyopo wilaya ya Rufiji mkoani Pwani ambayo inatoa elimu bure kwa watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi nia ya kuanzisha shule hii yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne 325 ni kuwapatia watoto hawa elimu sawa na wenzao ambao wanawazazi.
Kazi nyingine zinazofanywa na Taasisi hiyo ni kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kuwaongezea mitaji ya biashara na kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo wanatarajia kuwafikia wanawake 60000.
Pia wanahakikisha vifo vya kina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vinapungua kwa kutoa elimu kwa jamii jinsi gani inaweza kuepukana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa elimu ya jinsia na uzazi kwa vijana ili waweze kuepukana na mimba za utotoni na ugonjwa wa Ukimwi.
Akifungua mkutano huo Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia unyanyasaji wa kijinsia na utatuzi wa migogoro Zainabu Bangura alieleza kwamba katika bara la Afrika wanawake wanazalisha mali kwa asilimia 70 ya uchumi usio rasmi na asilimia 20 kwa uchumi rasmi hivyo basi kuwanyanyasa, kuwabagua, kuwakandamiza na kuwadidimiza wanawake ni sawa na kudidimiza taifa zima.
Msemaji Mkuu katika mkutano huo kutoka Umoja wa Afrika (AU) Aisha Abdullahi ambaye ni Kamishina anayeshughulikia masuala ya siasa alisema kuwa pamoja na ukweli kwamba ndani ya Bara la Afrika kuna utashi mkubwa wa kisiasa na nia ya kushughulikia changamaoto za masuala ya kibinadamu, bado bara hilo linakabiliwa na idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani na nje zaidi ya million 15.
Abdhullahi alisema, "Wakimbizi hawa wanahangaika kutafuta mavazi, chakula na makazi maeneo mbalimbali ya Bara la Afrika. Pamoja na changamoto nyingine za umaskini, uchumi duni na matatizo ya kisiasa katika baadhi ya nchi Umoja wa Afrika umeliweka suala la wakimbizi kuwa ni moja ya agenda zake muhimu".
Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi za umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za taasisi za kimataifa na kikanda. Chanzo: Anna Nkinda, Maelezo, Newyork

WAKAGUZI WA UN WA SILAHA ZA KEMIKALI WAREJEA SYRIA

sumu 644f4
Wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa wamerejea Syria kufanya uchunguzi wa matumizi ya silaha hizo zilizopigwa marufuku nchini humo wakati wa miaka miwili na nusu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. (HM)

Kundi linaloongozwa na Ake Sellstorm lilikwenda nchi jirani ya Lebanon jumatano na kusafiri kwa kutumia gari hadi Damascus.
Kwanza walikwenda Syria mwezi uliopita kufanya uchunguzi wa mashambulizi matatu ikiwemo lile la mwezi Machi nje ya mji wa Aleppo ambalo serikali ya Syria na wapiganaji waasi wanashutumiana.
Kundi hilo lilihamisha mwelekeo wake wa ujumbe wa wiki mbili na kuzingatia shambulizi jipya nje ya Damascus ambako waligundua kwamba silaha za kemikali zilitumika.
Wakati huohuo Jumatano kundi la waasi 13 lilitoa taarifa ya pamoja kupinga baraza la upinzani la taifa la Syria likisema kuwa haliwakilishi tena ushawishi wao.
Watu wengi waliokimbia nchi hiyo wamekwenda nchi jirani ikiwemo Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq. Chanzo: bbcswahili

UTPC YAJIPANGA KUISHTAKI SERIKALI KWA MAUAJI

karsan e3347
UMOJA Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umesema jopo la wanasheria wake lipo katika hatua za mwisho za kuandaa mashitaka dhidi ya Serikali kutokana na mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi. (HM)

Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan alipozungumza na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari kutoka Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Karsan alisema Serikali itafunguliwa mashitaka ya madai kwa kuwa askari wake ndiyo waliotekeleza tukio la kinyama dhidi ya Mwangosi wakati akitimiza majukumu yake.
"Baada ya tukio lile la Septemba 2,2012, UTPC hatukutaka kuanza kulumbana na Serikali bali tulianza kushughulikia kwanza familia ya marehemu Mwangosi ili kurudi katika hali yake ya kawaida.
"Tumefanikiwa kuiweka familia yake katika hali nzuri ya uchumi kwa kuanza kumwanzishia mke wake mradi wa zaidi ya Sh milioni 10 ambao anaendelea nao mpaka sasa, pia tuanzisha mfuko wa maalum wa Daudi Mwangosi Fund.
"Mfuko huu utakuwa maalum kwa waandishi wote watakaopatwa na matatizo ya aina yoyote yake, pia kila mwaka Septemba 2 tutakuwa tunatoa tuzo Sh milioni 10 kwa mwandishi bora.
"Sasa msimamo wa UTPC ni kutaka Serikali itoe malipo kwa familia ya marehemu Mwangosi, hatufungui kesi ya jinai la hasha kwa sababu hatua za sheria kwa askari waliohusika zinachukuliwa," alisema.
Mauaji ya Mwangosi yalitokea Septemba 2, 2012 eneo la Nyololo wa katika ufunguzi wa tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kuibuka ghasia polisi walipoamuru wafuasi wa chama hicho kutawanyika katika ufunguzi wa tawi hilo.
Katika hatua nyingine, UTPC imepiga marufuku waandishi wa habari kuomba au kupokea posho kutoka kwa wadau wa habari ispokuwa tu pale anapotoa kwa hiari yake. Chanzo: mtanzania

MMILIKI ARSENAL ASEMA WENGER ANABAKI ARSENAL 

wenger 24bf5
CHIFU wa Arsenal, Stan Kroenke anataka kocha Arsene Wenger abaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu na kuleta taji la Ligi Kuu ya Enland Emirates. (HM)
Mfaransa huyo amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 17 na The Gunners ikiwa inakabiliwa na ukame wa mataji kwa msimu wa tisa sasa, amekuwa akipigwa zengwe aondoke, hususan kutokana na Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.
Lakini mtu mwenye hisa nyingi za klabu, Kroenke hana shaka anataka Wenger abaki.
Mmarekani huyo amesema kwamba hafikiri kama kuna mwingine bora kuliko yeye na anaamini Wenger anafanya kazi nzuri.
Alipoulizwa kama mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 yumo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo, Kroenke alisema: "Hiyo ni sahihi kabisa. Arsene anafahamu ambavyo tunahisi, falsafa zetu ni nini, nini tunataka kufanya na ninahisi tuko pamoja sana,".
Kufuatia klabu kuvuna rekodi yake ya usajili kwa kumsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid.
Kroenke alisema: "Kwa kweli namfurahia Arsene - safi sana, mweledi. Ana upeo mkubwa wa uongoza timu na klabu. Yuko sahihi katika hilio.
Kroenke pia amesema Wenger hastahili lawama kwa klabu hiyo la Kaskazin mwa London kumkosa mshambuliaji Luis Suarez, kwani ni Liverpool ndio hawakuwa tayari kumuuza nyota huyo kutoka Uruguay. Chanzo: binzubeiry

Friday, September 27, 2013

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFUNGUA OFISI 23 KATIKA MIKOA MBALIMBALI

IMG_4793_6c790.png
Wakili wa serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Frederick Manyanda (kulia) akieleza kwa waandishi wa (hawapo pichani) mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu kwa kufungua ofisi zaidi Mikoani, Katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam,katikati ni Afisa Habari toka ofisi hiyo Bi. Asiatu Msuya na Kulia kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi. Georgina Misama.(P.T)
IMG_4776_c5f41.png
Afisa Habari, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Asiatu Msuya (kushoto) akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ufunguaji wa ofisi 23 katika mikoa mbalimbali nchini ili kutekeleza Mpango wa kutenganisha Upelelezi na uendeshaji wa Mashtaka, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Wakili wa serikali Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Frederick Manyanda.
PICHA NA HASSAN SILAYO> MAELEZO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFUNGUA OFISI 23 KATIKA MIKOA MBALIMBALI KUFANIKISHA MPANGO WA UTENGANISHWAJI WA SHUGHULI ZA UPELELEZI NA UENDESHAJI WA MASHTAKA NCHINI
______________________________
Utangulizi
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanikiwa kufungua Ofisi 23 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro (Moshi), Arusha, Mwanza, Kagera (Bukoba) Mara (Musoma), Shinyanga, Tabora, Singida, Iringa, Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma, Rukwa (Sumbawanga),Ruvuma (Songea), Njombe, Manyara,Morogoro,Kigoma,Geita na Pwani. Aidha jumla ya Ofisi mbili (2) za zimefunguliwa katika Wilaya za Temeke na Monduli. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 pekee jumla ya Ofisi tano (5) zimefunguliwa katika mikoa ya Pwani, Kigoma, Morogoro, Manyara, Njombe na Geita ikiwemo pia Ofisi mbili za Wilaya.
Lengo
Lengo kuanzishwa na kuimarishwa kwa Ofisi hizi za Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha kuwa huduma ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu zaidi. Baadhi ya huduma zinazotolewa ni pamoja na kuendesha Mashtaka mahakamani, kushughulikia malalamiko na kero za wananchi kuhusiana na kesi za jinai na madai zinazowakabili, kutembelea mahabusu na kuratibu upelelezi wa kazi za upelelezi wa makosa ya jinai zinazofanywa na vyombo pelelezi/chunguzi ikiwemo Polisi, Magereza, Uhamiaji,TAKUKURU.
Utekelezaji wa Mpango wa kutenganisha Upelelezi na Mashtaka nchini
Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kutekeleza mpango huu wa Utenganishwaji wa Upelelezi na Mashtaka kwa mujibu wa Sheria ambapo mfumo wa Sheria ambao uliwezesha kutungwa kwa Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, 2005 na Sheria ya Usimamizi wa Uendeshaji Mashtaka nchini, 2008 umeboreshwa; pamoja na kuanzishwa kwa Jukwaa la Ki-taifa la Haki-Jinai (National Criminal Justice Forum) Desemba 2009 linaloviunganisha pamoja vyombo vyote vinavyosimamia utolewaji wa Haki-Jinai nchini;
Serikali pia imeboresha Muundo wa Divisheni ya Mashtaka kwa kuweka Sehemu (Section) mahsusi inayosimamia utekelezaji wa mchakato wa utenganishaji wa kazi za upelelezi na Mashtaka na uratibu wa kazi za ki-pelelezi; pamoja na kuanzishwa kwa huduma ya Mashtaka ya moja kwa moja ambako Mawakili wa Serikali wanaendesha kesi; Hii imepelekea idadi ya kesi zinazofunguliwa Mahakamani ambako Mawakili wa Serikali wanaendesha Mashtaka kupungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma; Kuongezeka kwa ubora wa huduma zitolewazo na kupungua kwa kesi za kubambikizwa.
Utekelezaji wa Programu ya Utenganishwaji wa Mashtaka na Upelelezi (Civilianization) imetoa msukumo mkubwa kwa Ofisi kuingia uanachama na makubaliano ya mashirikiano na vyama vinavyohusiana na kazi za Uendeshaji Mashtaka duniani, kama vile-IAP, HOPAC, APA, EAAP, na ARINSA; Serikali itaendelea kupanua wigo wa uendeshaji wa Mashtaka kwa kuanzisha na kuimarisha Ofisi katika Wilaya zote nchini pamoja na Mikoa miwili iliyobaki ya Katavi na Simiyu.
Tunapenda kuwakumbusha Wadau wetu wote na Wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za uhalifu au jinai yoyote katika jamii kwa vyombo husika kupitia utaratibu unaofaa; na kutoa ushahidi Mahakamani pale unapohitajika kwa kuwa hizi ni nguzo muhimu katika uendeshaji wa kesi mbalimbali. Aidha tunatoa wito kwa umma, wadau wetu na wananchi wote kwa ujumla pamoja na vyombo vya habari nchini kufuatilia mtiririko, hoja zinazowalishwa Mahakamani na uamuzi uliotolewa na Mahakama katika kesi mbalimbali zinazoendelea kuwa na taarifa sahihi ya kuhusu kesi hizo.
Imetolewa Na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ijumaa, Septemba 27, 2013
Kwa mawasiliano zaidi
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
SLP 9050
KIVUKONI FRONT
DAR ES SALAAM
SIMU: +255 22 21181778
NUKUSHI: +255 22 2113236
BARUA PEPE: info@agctz.go.tz
TOVUTI: www.agctz.go.tz

Taarifa ya JKT kwa vijana wanaotaka kuahirisha mafunzo 

 JKT1_4a456.jpg

Vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT awamu ya tatu na pia wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu, wambao wanataka kuahirisha mkataba wa JKT, wanatakiwa kuandika barua Makao Makuu ya JKT kuomba kuahirisha mkataba wa JKT.(P.T)
1. Barua binafsi kuomba kuahirisha mkataba iwe na picha yake.
2. Nakala ya barua ya kucahguilwa kujiunga na chuo (Joining instructions)
3. Barua hiyo ieleze kuwa utajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo.
4. Barua zao zifike Makao Makuu ya JKT kabla ya tarehe 02 Kotoba, 2013.
ANGALIZO
Kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Hivyo ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.
Agizo hili limetolewa na Jeshi la Kujenga Tafia, Makao Makuu.
---
Imetolewa kwenye tovuti: http://jkt.go.tz/mkataba-jkt.html
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2g4C18z5v

Mabilioni yaliyofichwa Uswissi yaongezeka

 1-frederick_weremakulia_naibu_wziri_wa_habariu_na_Vijana_Amos_Makalla_ddb2b.png

Benki Kuu ya Uswissi imesema fedha za Watanzania zilizokuwa zimewekwa katika benki za nchi hiyo zimeongezeka kutoka Dola za Kimarekani 3.6 bilioni mpaka Dola 5.4 bilioni.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo kwenye Mtandao wa Reuters, zilisema kuwa fedha hizo zimeongezeka hivyo kwa kipindi cha kati ya mwaka jana na mwaka huu.
"Ingawa kiasi cha fedha hizo kimetofautiana kila mwaka kwa mwongo mmoja uliopita," inasema sehemu ya taarifa hiyo ya Reuters ambayo ilikuwa ikinukuu ripoti za Benki Kuu ya nchi hiyo.(P.T)
Hata hivyo, taarifa hizo hazikufafanua ni kwa nini fedha hizo zimeongezeka kwa kiasi hicho.
Taarifa za awali kutoka kwenye kamati ya Serikali inayochunguza mabilioni hayo, ilionyesha kuwa kuna uwezekano wa kuwapo kwa fedha nyingi nchini humo kuliko zile zilizotolewa na ripoti ya benki hiyo ya mwaka 2012 iliyosema kuwa kulikuwa na Dola za Marekani milioni 3.6.
Taarifa hizo zinasema mbali na fedha kuna uwezekano mkubwa wa Watanzania kuwa na nyumba na rasilimali nyingine walizowekeza nchini humo.
Januari 11, mwaka huu, Balozi wa Uswisi nchini,Olivier Chave, aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalumu kuwa hakuna jitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka ufumbuzi wa tuhuma za watu walioficha fedha nchini humo.
Siku chache baadaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema alizungumza na gazeti hili na kusema kuwa hawezi kumjibu chochote balozi huyo kwa kuwa ni mtu mdogo kwake.
"Najua kuwa huyu balozi ana kinga, ila siyo adabu hata kidogo kuzungumza maneno yale kwenye nchi ya watu. Kama ingekuwa ni balozi wa Tanzania huko Uswisi kasema maneno haya, angeambiwa tu arudi nyumbani kupumzika hadi watakapomhitaji," alisema Werema.
Werema alisema kwenye Bunge lililokaa Aprili mwaka huu wangekuwa na kitu cha kuwasilisha bungenijambo ambalo halikutimizwa.
Baada ya ukimya huo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alimwandikia Katibu wa Bunge barua akitaka Serikali iwasilishe majibu juu ya uchunguzi wa fedha hizo kwenye Bunge lijalo.
Gazeti hili lilipomtafuta Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah ili kujua kama amepata barua hiyo alisema kuwa "Mimi sijaipokea hiyo barua na nimetoka ofisini leo saa kumi na sikuiona, labda kama alimtuma mtu na amekaa nayo."
Kwa upande wake Zitto alisisitiza kuwa "Hiyo barua nimeipeleka leo (jana) saa tano na kawaida tunazipeleka masijala ndiyo wampelekee, hatumpi katibu mkononi moja kwa moja."
Chanzo:Mwananchi

Warioba: Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ina upungufu 

warioba_16def.jpg
Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.
Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.(P.T)
Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa Katiba Mpya.
Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu, muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: "Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni?"
Jaji Warioba pamoja na kukiri upungufu huo, alisema kurekebisha au kutokurekebisha kasoro hizo si jukumu la tume hiyo.
"Tunawaomba watafakari, waone jinsi gani tume ambayo imekwishavunjwa itakuja kutoa elimu wakati wa kura ya maoni, sheria ina 'contradiction' (ina mkanganyiko)," alisema.
Muswada huo ulipitishwa na wabunge wa CCM baada ya wale wa upinzani kutoka nje baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe kuamuriwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutoka nje kutokana na kukaidi kwake amri ya kukaa chini alipokuwa akitaka kutoa hoja kabla ya mjadala wake kuanza.
Muswada huo unapingwa kwa kuwa Rais amepewa mamlaka ya kuteua wajumbe 166, ambao si wabunge wala wawakilishi na Zanzibar kutokushirikishwa kikamilifu kwenye maandalizi ya muswada huo.
Hata hivyo, Warioba alisema pamoja na kasoro hizo Tume hiyo inafanya kazi yake kwa kufuata sheria hiyo huku akisisitiza, "Wanaotunga sheria ni wengine siyo sisi, tulipoteuliwa tulikuta sheria na kuanza kazi kwa kuifuata. Imefanyiwa marekebisho sisi tunafuata."
Alisema waliofanya mabadiliko ya sheria hiyo wana haki ya kufanya hivyo na kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haiwezi kuzuia kutokufanyika kwa mabadiliko hayo, kwani yapo baadhi yanaihusu.
Alisema baada ya kuipata sheria hiyo: "Tulijiuliza maswali kwa sababu miswada huwa inapelekwa bungeni na Serikali ikiwemo ya Katiba. Anayeipeleka kama ni waziri ndiye anayetoa ufafanuzi pale inapohitajika."
Alisema kulingana na sheria, tume yake ndiyo inayotakiwa kutoa ufafanuzi katika Bunge la Katiba, kama ambavyo Waziri hutoa maelezo anapowasilisha muswada bungeni.
"Tulipouliza tulielezwa kwamba sisi ambao tumepewa jukumu la kupata maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ndiyo tutaitwa pale tu patakapohitajika ufafanuzi wa jambo fulani," alisema.
Alisema kazi ya kuandaa Rasimu ya Katiba itafanyika na kukamilika katika muda uliopangwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
"Tulianza kazi Mei mwaka jana na tunatakiwa kumaliza Novemba mwaka huu, sheria inaruhusu kuongeza miezi miwili kama tutakuwa hatujakamilisha kazi. Katiba Mpya inatakiwa iwe imekamilika Aprili 26, 2014," alisema.
Chanzo:Mwananchi

Kenya yamsaka Samantha Lewthwaite 

nairobi c0494
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani. (HM)

Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.

Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol, mwanamke huyo anasakwa na serikali ya Kenya kwa kumiliki mabomu na kupanga njama ya kufanya mashambulizi kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa mwanamke huyo atakamatwa katika nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa na kusibiri kupelekwa katika nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa dhidi yake.
Bi Lewthwaite anajulikana kwa jina bandia la, "Natalie Webb" –na alikuwa anasakwa kwa madai ya kumiliki hati bandia ya usafiri nchini Afrika Kusini.
Ni mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa washambuliaji wanne waliohusika na shambulizi la kigaidi mjini London ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa. Chanzo: bbcswahili

YANGA YAWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA 

nsajigwa faa6e
Baada ya vuta ni kuvute huku ikitishiwa kulimwa adhabu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), klabu Yanga imekubali matokeo na kumalizana na wachezaji wake wa zamani, Stephano Mwasika na Shadrack Nsajigwa 'Fusso' waliokuwa wakiidai klabu hiyo zaidi ya Sh15 Milioni. (HM)


Wachezaji hao walikuwa wanaidai Yanga fedha hizo kutokana na malimbikizo ya ada ya usajili, ambapo uongozi wa klabu hiyo ulikuwa ukiwapiga danadana kuwalipa wakati walipokuwa waikiitumikia.


Kutokana na hali hiyo wachezaji hao baada ya kuachwa na klabu hiyo katika usajili wake wa msimu huu waliamua kuishtaki Yanga ili iweze kuishinikiza na kuwalipa haki zao.


Nsajigwa, alikuwa akiidai Yanga kiasi cha Sh 9 milioni wakati Mwasika ambaye sasa anaitumika Ruvu Shooting alikuwa akiidai Yanga Sh 6.5 milioni.


Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameliambia gazeti hili jana kuwa wamemalizana na wachezaji hao siku tatu zilizopita.


Alisema Yanga haikuwa na nia ya kuwadhulumu wachezaji hao isipokuwa malipo yao yalichelewa kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali za kiutawala.


"Tumemalizana nao, lakini ni vema ukawauliza na wenyewe kwa uhakika zaidi," alisema Mwalusako.


Hata hivyo Nsajigwa alipouliwa alikubali kuwa tayari wamemalizana na klabu hiyo tangu siku ya Jumatatu na sasa hana kitu chochote anachoidai klabu hiyo. Chanzo: Mwananchi

AL-QAEDA YAITISHA TANZANIA

al qaeda somalia 1058704051 919f8
*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi
WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.(HM)


Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana.

Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio mengine Tanzania na Uganda.

Babile alisema taarifa zinaonyesha vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa watapata utajiri wa haraka.
Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.
"Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao... tumejipanga kuyakabili haya na kuushirikisha umma katika ulinzi," alisema.
Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote litakalotokea.
"Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.
"Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline officers wetu wako makini mno.
"Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.
"Lakini hata kwenye mipaka yetu yote hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama," alisema.
Baada ya kufanya mashambulio mjini Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.
Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho yataelekezwa Uganda na Tanzania.
Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate.
Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.
"Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi, tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha hakuwa mtu hatari, tukamuachia.
"Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea... lakini tumeangalia taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka," alisema Babile. Chanzo: mtanzania

LEWANDOWSKI KUSAINI BAYERN MUNICH JANUARY - MWENYEWE ATHIBITISHA 

 bayern 2e8de

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amethibitisha rasmi kwamba atasaini mkataba wa kwanza wa makubaliano wa kujiunga na Bayern Munich katika soko la usajili la mwezi wa January kisha kujiunga na mabavaria mara tu mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu. (HM)

Baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu mshambuliaji huyu wa kipoland, hatimaye hivi sasa ipo wazi Pep Guardiola atamuongeza mshambuliaji katika kikosi chake 2014.

Kwa mara ya kwanza mchezaji amekiri kwamba atajiunga na Bayern mwishoni mwa msimu wakati alipokuwa akihojiwa na Sport 1, alisema: 'Ndio, nathibithisha nitahamia Bayern kwa sababu sasa hivi nikasaini mkataba wa makubaliano.' Chanzo: sportmail

TP MAZEMBE KUANZA NA STADE MALIEN, FAINALI ZA AFRIKA

 samatta mputu na ulimwengu1 f3ffc

TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), itaanzia ugenini Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stade Malien ya Mali, Oktoba 6, mwaka huu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Lubumbashi. (HM)


Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jana, mchezo wa kwanza utachezwa kwenye Uwanja wa Modibo Keita mjini Bamako kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za huko na saa 12:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Mechi hiyo itachezeshwa na refa Alioum Neant, atakayesaidiwa na Evarist Menkouande wote wa Cameroon na Peter Edibi wa Nigeria, wakati refa wa akiba atakuwa Mohamadou Mal Souley pia wa Cameroon.

Timu hizo zitarudiana Oktoba 19, Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, zikichezeshwa na marefa Haimoudi Djamel wa Algeria atakayesaidiwa na Achik Redouane wa Morocco na Etchiali Abdelhak wa Algeria, wakati refa wa akiba atakuwa Bousseter Sofiane wa Algeria pia.


Mazembe inayoongozwa na washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu, ikifanikiwa kuitoa Stade Malien itamenyana na mshindi wa Nusu nyingine, kati ya timu za Tunisia tupu, Club Africaine na C.S. Sfaxien.


Ikumbukwe Mazembe iliangukia kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na sasa inaelekea kufuta machungu kwa kutwaa taji hilo la pili kwa ukubwa kwa michuano ya klabu Afrika. Chanzo: binzubeiry

NCHI ZA MAGHARIBI KUZUNGUMZA NA IRAN

zzzzgermany_62b38.jpg

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi tano wanachama wa baraza la usalama la umoja Mataifa na Ujerumani watakutana na mwenzao wa Iran leo kuzungumzia jinsi ya kutatua mzozo wa mpango wa kinyuklia wa Iran
Mkutano huo utakaofanywa pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la umoja wa Mataifa mjini New York, unanuia kutoa fursa kwa duru ya kwanza ya mazungumzo yenye tija pengine mwezi ujao tangu ya mwisho yaliyofanyika mwezi Aprili.
Mkutano wa leo pia utakuwa wa kwanza wa ngazi ya juu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani,John Kerry, kukutana ana kwa ana na mwenzake wa Iran, Javad Zarif, kwani nchi hizo mbili hazijaweza kukaa chini pamoja kwa miaka mingi sasa kufuatia uhasama wa kidiplomasia.(P.T)
Mkutano kipimo cha azma ya Iran
Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, China na Ujerumani zitashiriki katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya, Bi Catherine Ashton. Urusi na China pia zinatarajiwa katika mkutano huo.
Haya yanawadia kufuatia kufufuliwa kwa matumaini ya kupatikana ufumbuzi wa mzozo huo wa mpango wa kinyuklia baada ya rais mpya wa Iran, Hassan Rouhani, aliye na msimamo wa wastani, kuashiria kuwa nchi yake iko tayari kwa mazungumzo na nchi za magharibi.
Rais wa Marekani, Barrack Obama, amemuagiza Kerry kushughulikia uwezekano wa kufufuliwa kwa mazungumzo yatakayotatua mzozo huo wa kinyuklia na kusisitiza kuwa Iran sharti ithibitishe kuwa kweli ina nia ya kupatikana kwa suluhisho.
Rouhani mapema wiki hii katika hotuba yake ya kwanza katika baraza la umoja wa Mataifa alisema nchi yake haina cha kuficha kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia kwani lengo lao sio kuwa kitisho kwa ulimwengu.
Palipo na nia pana njia
Kiongozi huyo wa Iran amesema iwapo kuna nia ya kisiasa kutoka nchi za magharibi basi nchi yake iko tayari kwa mazungumo na anaamini kuwa mzozo huo unaweza kutatulika kupitia mazungumzo hayo.
Rouhani ameongeza kuwa anatarajia makubaliano kuafikiwa katika kipindi cha miezi mitatu au sita ijayo na kusisitiza kuwa azma yake hiyo inaungwa mkono na kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ali Khamenei.
Ashton amesema amefurahishwa na azma na juhudi za waziri wa mambo ya nje wa Iran lakini akaongeza mengi bado yanahitajika kufanywa.
Nchi hizo za magharibi zilitoa pendekezojipya kwa Iran mapema mwaka huu kabla ya kuchaguliwa kwa Rouhani linaloaminika kuwa lina lengo la kulegeza vikwazo vilivowekewa nchi hiyo na kuathiri uchumi wake na badala yake Iran ipunguze uzalishaji wake wa madini ya Uranium.
Mwandishi:Caro Robi/afp/ap

Thursday, September 26, 2013

MANJI AWATULIZA WACHEZAJI YANGA 

Manji 21 84226
MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji amewaambia wachezaji wa timu hiyo kwamba hana matatizo nao kwa matokeo ya awali ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na amewataka waelekeze nguvu zao katika mechi zijazo.(HM)


Yanga imeambulia pointi sita katika mechi tano za awali za Ligi Kuu ya Vodacom, kutokana na sare tatu, kushinda moja na kufungwa moja, hivyo kuachwa kwa pointi tano kileleni na wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
Jana Manji alikutana kwa chakula cha jioni na wachezaji wa timu hiyo katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam akiwa ameambatana na Makamu wake Mwenyekiti, Clement Sanga, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji na Mjumbe wa Sekretarieti, Patrick Naggi.
Katika kikao hicho, Manji aliwaambia wachezaji wa Yanga hamlaumu yeyote kwa matokeo hayo, kwani ligi bado mbichi, ila akawataka waunganishe nguvu zao kuelekea mechi zijazo, ili kurejesha ushindi na furaha klabuni.
Pamoja na hilo, Manji alizungumzia suala la madai ya baadhi ya
wachezaji ya fedha za usajili na akaliweka sawa kwa wale ambao walikuwa wanadai kuwawekea utaratibu wa malipo haraka, jambo ambalo Naggi ametakiwa kuhakikisha analishughulikia mara moja.

Aidha, Manji baada ya kikao cha pamoja na wachezaji wote, alimvuta pembeni Mrisho Ngassa kujadiliana naye faragha.

Haikujulikana mara moja Manji alizungumza nini na Ngassa, lakini inaweza kuwa kuhusu deni analotakiwa kuilipa Simba SC, Sh. Milioni 45 kwa kosa la kusaini Mikataba na timu mbili. Ngassa alifungiwa mechi sita za mashindano na kutakiwa kurejesha fedha alizochukua Simba SC Sh. Milioni 30 pamoja na fidia ya Sh Milioni 15.

Habari za ndani zinasema, Yanga SC inaweza kulipa deni hilo ili Ngassa aanze kucheza, lakini italazimika kurejeshewa fedha hizo na mchezaji mwenyewe, kwa kuwa klabu ilikwishamalizana naye katika usajili wake.

Kuna uwezekano deni hilo likatumika kumuongezea Mkataba Ngassa Yanga SC kutoka wa miaka miwili aliosaini sasa. Ngassa mwenyewe hakupatikana alipotafutwa leo kuzungumzia suala hilo.

Yanga SC itamenyana na Ruvu Shootings Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa ligi hiyo, wakati leo Rhino Rangers wanaikaribisha Ashanti United Mwinyi, Tabora.

Mechi nyingine zitapigwa Jumapili, Simba SC ikishuka dimbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na JKT Ruvu, Rhino Rangers na Kagera Sugar Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, Mbeya City na Coastal Union Sokoine, Mbeya, Mgambo JKT na JKT Oljoro Mkwakwani, Tanga na Ashanti United na Mtibwa Sugar, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Chanzo: binzubeiry

Ni al-qaeda, si al shabaab

westgate 870d9
  • Magaidi wa Marekani, Uingereza, Syria wahusika
SHAMBULIO la kigaidi lililofanywa nchini Kenya Jumamosi iliyopita na watu waliodhaniwa kuwa wafuasi wa Al- Shabab, sasa limeelezwa kutekelezwa na mtandao mpana zaidi wa kigaidi wa kundi la Al-Qaeda. (HM)

Baadhi ya wachambuzi na wachunguzi wa masuala ya kiusalama na kimataifa, wameyataja mambo matatu ambayo yanathibitisha pasipo shaka kwamba waliotekeleza tukio hilo la kuvamia, kuteka nyara na kuua watu wapatao 68 katika Kituo cha Biashara cha Westgate, ni wa aina ya kundi ambalo kinadharia na kimatendo linafanana na lile la kigaidi duniani la Al-Qaeda. Mambo yanayotajwa na wachambuzi na wachunguzi hao ni pamoja na mbinu, teknolojia na aina ya watu waliotumika kutekeleza shambulio hilo.
Katika uchambuzi wao, wameeleza kuwa mbinu iliyotumiwa na magaidi hayo kuvamia pasipo kujulikana mara moja na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchini Kenya, lakini pia aina ya silaha walizokuwa nazo, inaonyesha kuwa kundi hilo limeamua kutumia kivuli cha Al-Shabab kufikisha ujumbe kwa dunia kwamba lipo licha ya uongozi wake kubadilika.
Kwamba mbali na mbinu pamoja na teknolojia, pia aina ya watu waliohusika kutekeleza shambulio hilo ambao wamebainika kutoka katika mataifa mbalimbali duniani, ndio ambao wamewafanya wachambuzi na wachunguzi hao waanze kupata shaka kwamba huenda kuna kundi kubwa zaidi lililotekeleza shambulio hilo, ambalo limejivika taswira ya Al-Shabab.
Watu wanaotajwa kuvamia kituo hicho cha biashara na kutekeleza unyama wa kutisha, wanaelezwa kutoka katika mataifa ya Somalia, Uingereza, Marekani na Syria.
Taarifa hizi zinathibitishwa na kauli iliyotolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed ambaye katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera, alisema kuwa Al-Shabab hawakuwa peke yao katika shambulio hilo.
Mohamed aliiambia Al - Jazeera kuwa al-Qaeda ndio waliokuwa nyuma ya tukio hilo na si Al-Shabab.
"Al-Shabab hawafanyi peke yao, hili shambulio ni sehemu ya kampeni ya ugaidi wa kimataifa," alisema Mohamed.
Waziri huyo alisema zaidi ya magaidi 20 wakiwemo wanawake, walikuwa nyuma ya shambulio hilo na kwamba watu hao wametoka katika mataifa tofauti tofauti duniani.
"Al-Shabab wanataka kujionyesha kwenye ngazi ya kimataifa, hasa baada ya kubadili uongozi na wanataka kuionyesha dunia kwamba wana nguvu bado, hivyo kuwekwa kwenye kundi la kulifikiria," alisema.
Katika mahojiano yake mengine na kituo cha cha PBS cha nchini Marekani, Waziri Mohamed alisema washambuliaji kama wawili au watatu wamebainika kuwa ni raia wa Marekani na Mwingereza mmoja.
Ni kutokana na taarifa hizo, baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa shambulio hilo la kigaidi lina ajenda zaidi ya Kenya.
Zipo hisia kwamba shambulio hilo halikuwa na lengo la kuiumiza Kenya pekee, kutokana na hatua yake ya kupeleka majeshi yake kwenda kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabab nchini Somalia, bali pia kumuumiza Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye kwa asili anatoka nchini humo.
Obama ambaye nchi yake imekuwa ikiongoza mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi ikiwamo lile la Al-Qaeda, ambapo hivi karibuni ilifanikiwa kumuua kiongozi wake, Osama bin Laden, baba yake ni raia wa Kenya.
Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa, kitendo cha magaidi kuamua kukishambulia kituo hicho cha biashara cha Westgate, kinatokana pia na ukweli kuwa watu wengi wanaopenda kutembelea hapo ni raia kutoka mataifa ya Magharibi wakiwemo Wamarekani, hivyo ulikuwa ni mkakati wa kumuumiza Obama kwa njia hiyo.
Katika hotuba yake aliyoitoa siku ya Jumatatu, Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, alilielezea kundi la Al-Shabab kuwa ni tishio jipya kwa dunia. Chanzo: mtanzania