WAANDAMANAJI NCHINI MISRI HAWATISHIKI
WAFUASI
wa Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi -- wamekataa
wito uliotolewa na wizara ya mambo ya ndani kumaliza maandamano yao
katika medani mbili kubwa za mjini Cairo.
Msemaji wao Alaa Mostafa amesema maandamano yao yataendelea.
Wizara iliwataka waandamanaji kuondoka
na kuwapa fursa ya kuwalinda wakati wakiondoka na ahadi ya kutowapeleka
mahakamani iwapo watatii maelekezo ya wizara hiyo. (HM)
Jumatano serikali inayoungwa mkono na
jeshi nchini humo iliamuru polisi kuwatawanya waandamanaji walioweka
kambi katika midani hizo.
Bw. Morsi Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia aliondolewa na jeshi mwezi mmoja uliopita. Marekani imeitaka Misri kuheshimu uhuru wa kukutana ikiwemo kuweka kambi katika maeneo ya mikusanyiko. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment