LIST YA MASTAA WA BONGO WALIOFANYA/WANAOFANYA KAZI KAMA BALOZI WA MAKAMPUNI MAKUBWA
Unaambiwa vyanzo vikubwa vya pesa kwa wasanii wakubwa huko Ulaya
na Marekani ni udhamini wa kutoka kwenye makampuni mbalimbali ambayo
huwapa mastaa hao kazi ya kutangaza bidhaa fulani za kampuni yao au kuwa
balozi kamili wa kampuni nzima.
Moja ya mafanikio makubwa ni pale unapomuangalia P.Diddy ambaye
anaingiza pato kubwa sana akiwa anafanya kazi na Vodka ya Ciroc ambayo
ni mali ya kampuni kubwa ya vinywaji duniani Diageo.
Tukirudi Tanzania kuna makampuni ambayo yamesha amini nguvu na nafasi ya wasanii kwenye kuzitangaza bidhaa zao japokuwa bado wasanii wanaendelea kupeleka kilio chao mbele kama alivyofanya Ommy Dimpoz kwenye Kili Music award wakati anapokea tuzo yake.
Hii ni list ya watu maarufu Tanzania ambao waliweza kupewa na wengine wanaendelea hadi sasa hivi kufanya kazi na brand ili kufikia malengo ya kibiashara na kijamii ya brand hizo.
MWANA F.A NA SAMSUNG
Sio muda mrefu sana umepita tangu Samsung Tanzania kumtangaza Mwana F.A kama balozi wa bidhaa za Samsung , ni msanii ujazo wa jina lake uliongezeka kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye sanaa kwa miaka mingi.
B12 NA REDBULL
Hamisi mwingine huyu baada ya Hamisi Mwinjuma, kati ya watu maarufu wa kwanza sana kipindi hicho kupewa kazi ya kuwa balozi wa kinywaji cha Redbull akiwa anafanya show miongoni mwa show zinazosikilizwa sana na vijana.
B12 au Hamisi Mandi alikuwa balozi wa RedBull kwa muda ambako
kulipelekea kuitwa B-Balozi ambapo pia siku kadhaa zilizopita kutokana
na ukubwa wa kazi zake, uzoefu na hata uhodari, B12 hivi karibuni
alitajwa na kituo maarufu cha TV Afrika Kusini (Channel O) kama mmoja
kati ya Watangazaji 10 hodari wa Afrika akiwa kwenye namba 9.
MAREHEMU KANUMBA NA STARTIMES
R.I.P The great pioneer kama alivyokuwa anajiita, jina lake jingine
ni balozi wa Star Times ambapo kampuni hii ya ving’amuzi wakati inaingia
kwenye soko la Tanzania ilitumia pia mbinu ya kimasoko kwa kumtumia
mmoja kati ya watu maarufu kwenye TV.
Baada ya kufanya tamthilia kwa muda mrefu na baadae kuhamia kwenye
movie na kufanya vizuri zaidi, Kanumba alijipatia hili dili na
kulifanyia kazi vizuri…. alizunguka mikoa mbalimbali kwenye ziara za
kuhamasisha bidhaa ya Startimes huku picha zake zikionekana kwenye
mabango mbalimbali.
MZEE MAJUTO NA SHARO – AZAM
Marehemu Hussein Mkietti maarufu kama Sharo millionea akiwa pamoja na Mzee Majuto walipata dili tofautitofauti kutoka kwenye makampuni makubwa, matangazo ya Airtel lakini pia walipata nafasi ya kuwa mabalozi wa Azam.
Marehemu Hussein Mkietti maarufu kama Sharo millionea akiwa pamoja na Mzee Majuto walipata dili tofautitofauti kutoka kwenye makampuni makubwa, matangazo ya Airtel lakini pia walipata nafasi ya kuwa mabalozi wa Azam.
Kwa wale waliowahi kwenda sabasaba mwaka 2012 kwenye banda la Azam
waliwaona Mzee Majuto na Sharo millionea wakiwa nje ya banda hilo katika
kazi ya Azam ambapo Mzee Majuto alisema “Mkataba wetu na Azam ni mzuri
na tunamshukuru mungu kwa hili., mkataba wetu unasema tutahusika kwenye
kutengeneza matangazo ya bidhaa za Azam, promotion za wazi pamoja na
kupewa udhamini kama tukifanya shughuli yetu ya pamoja na mwanangu
Sharo”.
Hii ilikuwa kabla ya Sharomillionea kufariki ambapo baada ya Sharo kufariki bado Mzee Majuto anaendelea kazi ya Azam.
AMBWENE YESAYA (A.Y) NA AIRTEL
Boss wa Unity Entertainment mmiliki wa hits kama “Raha tu” “leo”
mpaka ‘bila kukunja goti’ & FA… alisain mkataba kufanya kazi na
Airtel Tanzania, kama Mzee Majuto na Sharo walivyofanya matangazo ya
Airtel na baadaye kupata dili jingine na Azam. A.Y aliwahi kufanya
tangazo la T.V, Radio na printing aki-promote moja bidhaa za Vodacom
Tanzania. Lakini baadaye baadaye sana akapata dili la kufanya kazi na
Airtel…. ambapo pia sasa hivi ni balozi wa moja kati ya vinywaji maarufu
duniani.
ADAM MCHOMVU NA COCACOLA
Mtangazaji wa XXL na Bongofleva Clouds FM AD aliwahi kuwa balozi wa Cocacola.
Mtangazaji wa XXL na Bongofleva Clouds FM AD aliwahi kuwa balozi wa Cocacola.
DIAMOND PLATINUMZ NA COCACOLA
Huyu jamaa anajiita Coca Boy, kama unataka kujionea hilo nenda kwenye account ya Instagram utaona pia ni jinsi gani anautendea haki ubalozi wake, Diamond ambae ni mmiliki wa nafasi za juu kwenye chati za muziki wa bongofleva kwa muda mrefu akiwa kwenye interview na XXL aliwahi kusema “Mimi nilipata nafasi ya kufanya tangazo la mashindano ya Cocacola, lakini nilikuwa na malengo na nikaamua kuwapa zaidi, bei niliyolipwa ni zaidi ya milioni 100 kwenye huu mkataba’
Huyu jamaa anajiita Coca Boy, kama unataka kujionea hilo nenda kwenye account ya Instagram utaona pia ni jinsi gani anautendea haki ubalozi wake, Diamond ambae ni mmiliki wa nafasi za juu kwenye chati za muziki wa bongofleva kwa muda mrefu akiwa kwenye interview na XXL aliwahi kusema “Mimi nilipata nafasi ya kufanya tangazo la mashindano ya Cocacola, lakini nilikuwa na malengo na nikaamua kuwapa zaidi, bei niliyolipwa ni zaidi ya milioni 100 kwenye huu mkataba’
Kwenye sentensi nyingine Diamond anakwamba ‘nilijifanya kama balozi
wakati kabla sijawa balozi kamili, kwa hiyo jamaa wakaona duh huyu jamaa
hatujampa hii kazi anafanya hivi je tukimpa kazi itakuwaje? hapo ndio
nikapata hii kazi”
No comments:
Post a Comment