TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, August 6, 2013

MOTO WATEKEZA UWANJA WA NDEGE WA KENYA 

K1 03646
K2 c552c
K3 1a99f

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi. Kwa sasa moto huo umeweza kudhibitiwa
Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo na anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa hakuna ripoti zozote za majeruhi .
Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.
Mamlaka ya uwanja huo imesema kuwa tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa.
Imesema kuwa baadhi ya operesheni za uwanja huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa kutua katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam ,Kigali, Mombasa na kwingineko nchini Kenya.
Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia zimeahirishwa.
Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.
Huu ni moto mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika uwanja wa Jomo Kenyatta wenye kutumiwa na wasafiri wengi zaidi katika eneo la Afrika mashariki na kati .
Taarifa za awali zilionyesha kuwa moto huo ulianzia kwenye eneo la uhamiaji katika kitengo cha kupokea wageni kabla ya kusambaa hadi maeneo ya ushuru na mizigo ya abiria.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana , lakini maafisa wa ngazi ya juu wa serikali wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta wametembelea uwanja huo na kutoa wito uchunguzi ufanyike mara moja. Hata hivyo hawakutoa ishara yoyote ni lini uwanja huo utafunguliwa tena .
Shirika la ndege la kenya -Kenya Airways, ambalo ni kubwa zaidi katika kanda ya Afrika limefuta safari zake zote na kuelekeza ndege zinazoingia nchini katika mji wa Mombasa . Tayari hisa za ndege zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 2 . Ndege za kimataifa ambazo zilitakiwa kuondoka leo asubuhi ziliruhusiwa kuondoka bila wasafiri.
Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment