China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini
Uwanja wa ndege unaojengwa na China katika visiwa vya Spatry
Marekani imetaka kuwepo usitishwaji wa ujenzi wa miradi kwenye maeneo yanayozozaniwa katika bahari ya kusini mwa China.
Waziri wa
ulinzi wa Marekani Ash Carter aliuambia mkutano mkuu wa ulinzi nchini
Singapore kuwa tabia ya China eneo hilio imekiuka sheria za kimataifa
Carter amesema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
Matamshi
yake yanakuja siku moja baada ya makao makuu ya jeshi la marekani kusema
kuwa china imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo.
Bwana
Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi . Hata hivyo amesema
kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.BBC
No comments:
Post a Comment