Kiwanja cha Ndege (JNIA) chatakiwa kuimarishwa kiushindani
Mshauri
Mkaazi wa ujenzi wa jengo la kufikia abiria katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi
ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri (Kulia) maendeleo mradi
huo.
Mwonekano
wa jengo la kushushia na kupandiashia abiria linaloendelea kujengwa
katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Uongozi
wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika
ujenzi unaoendelea wa jengo la kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyere (JNIA).
Ujenzi
huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita
katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu
za abiria kupandia na kushuka kwenye ndege, ofisi za uhamiaji na huduma
zingine muhimu.
Mkurugenzi
mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Suleiman S. Suleiman amesema kiwanja cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hapo awali kilikuwa na uwezo wa
kuruhusu ndege sita tu kutua kwa saa lakini kwa sasa unaweza kuruhusu
ndege hadi 30. Tunatarajia kuongeza ndege zaidi na hivyo kuufanya
kiwanja hiki kuhimili 2500 tofauti na abira 700 wa awali pindi ujenzi
huu utakamilaka.
Kwa sasa
ujenzi umefikia asilimia 85, katika awamu ya kwanza ambayo inategemewa
kukamilika Juni mwaka 2016 na itakiwezesha JNIA kuhudumia abiria milioni
tatu na nusu kwa mwaka. Iwapo ujenzi wa awamu ya pili utakamilika mwaka
2017 JNIA kitakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria milioni sita
kwa mwaka.
Alipokuwa
akitembelea mradi huo, Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango Bibi. Florance Mwanri, aliuambia uongozi wa Mamlaka hiyo
kuzingatia wazo la kuwa na huduma zote za msingi katika kiwanja cha
Julius Nyerere ili kuweza kushindana viwanja vya nchi jirani na barani
Afrika kwa ujumla.
"Ni vema
kuwa kiwanja chetu cha ndege kinapanuliwa ili kiweze kuhudumia watu
wengi zaidi, lakini nimegundua kuna vitu muhimu vimesahaulika katika
usanifu wa upanuzi huu, kuna vitu kama hoteli, jengo la hospitali,
sehemu za kupata huduma za kibenki na pia namna nzuri ya kuwapatia
abiria watuao usafiri wa kwenda mjini na sehemu nyinginezo, nadhani haya
pia yazingatiwe, alisema Bibi. Mwanri.(Muro)
No comments:
Post a Comment