Ugaidi ni tishio la Dunia:Nasrallah
Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah
Kiongozi
wa harakati za Shia wa Hezbollah Hassan Nasrallah amesema dunia
inakabiliwa na hatari kubwa kuwahi kutokea katika historia kutokana na
makundi ya kigaidi ya Islamic State na Al-Qaeda yanayopigana nchini
Syria .
Kauli
hiyo imekuja muda mfupi baada Waziri wa ulinzi wa Marekani kuyashutumu
majeshi ya Iraq kwa kukosa ari ya kupambana na wapiganaji wa Islamic
State.
Akihutubia
maefu ya wafuasi wake kwa njia ya video kiongozi huyo wa Hezbollah
Sheikh Nasrallah amekiri kwa mara ya kwanza kuwa Hezbollah imekuwa
ikipigana muda wote maeneo ya jirani na Syria kumsaida Rais wa Syria
Bashar al-Assad.
"Kila mtu
anapaswa kuona kuwa yupo kwenye hatari,na wala hii si hatari kwa wale
wanaolengwa na wapiganaji hao tu, ama Lebanon,Serikali ya Iraq na
makundi ya Yemen, hapa hii ni hatari kwa kila mmoja. Hakuna atakayezika
kichwa chake ardhini kuepuka mapigano hayo, ndiyo tunapigana kwaajili ya
ndugu zetu wa Syria,jeshi na wakazi wa Syria katika miji ya Aleppo,Homs
,Deir Ezzor ,Qalamoun,Hasakeh na Idlib".anasema Shekh Nasrallah
Naye
Waziri wa ulinzi wa Marekani,ameyashutumu majeshi ya Iraq kwa kukosa
morali ya kupambana na wapiganaji wa Islamic State. Katika hali
isiyokuwa ya kawaida ya maoni hayo ya lawama,Ash Carter amesema kwamba
majeshi yao yana idadi kubwa ya askari katika mji wa Ramadi,lakini
yalikumbana na upinzani walipokuwa wakishambulia na matokeo yake
walitimuliwa mjini humo. Akihojia na televisheni ya CNN Ash Carter
hakuna msaada wowote kwa majeshi ya Iraq.BBC
No comments:
Post a Comment