RAIS FILIPE NYUSI WA MSUMBIJI KULIHUTUBIA BUNGE LA TANZANIA.
Na.Aron Msigwa
Rais wa
Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi anatarajia kuwasili nchini Tanzania
Mei 17 mwaka huu kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo
mengine anatarajia kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.
Akitoa
taarifa ya ziara hiyo leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Said Mecki Sadiki amesema kuwa Rais Filipe Nyusi atawasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
slaam, Mei 17,2015 majira ya saa 6.
Amesema
mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais huyo atalakiwa na viongozi
mbalimbali wa Serikali, kupata mapokezi ya burudani ya ngoma za asili na
kukagua gwaride la heshima litakaloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzanian(JWTZ) na baadaye kupigiwa mizinga 21.(P.T)
Mhe.Sadiki
amesema kuwa mara baada ya shughuli ya mapokezi ya Rais huyo uwanja wa
ndege ataelekea Ikulu ambako atapokewa rasmi na mwenyeji wake,Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na baadaye viongozi
hao wawili watakua na mazungumzo ya faragha.
Amesema
Mei 18, 2015 Rais Filipe Nyusi atafanya mazungumzo na wafanyabiashara wa
Msumbiji waishio nchini Tanzania na kisha kuendelea na ziara yake
Visiwani Zanzibar ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
Ameeleza
kuwa baada ya kukamilisha ziara yake kisiwani Zanzibar Mei, 19 mwaka
huu, Rais Filipe Nyusi ataelekea mjini Dodoma ambako atakutana na
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Rais Jakaya Mrisho Kikwete yalipo
Makao Makuu ya Chama cha hicho na baadaye ataelekea Ukumbi wa Bunge
kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema
,Mhe.Filipe Nyusi atahitimisha ziara yake na kurejea nchini kwake Mei
19,2015 na kuwaomba wananchi hususan wakazi wa jiji la Dar es salaam
kuwa wavumilivu kutokana na usumbufu utakaotokana na baadhi ya barabara
zikiwemo Nyerere, mzunguko wa Kamata, Barabara ya Sokoine ,Luthuli na
Barabara ya Kilwa kufungwa mara kwa mara kupisha msafara wa kiongozi
huyo.
No comments:
Post a Comment