Majeshi ya Hamas yalaumiwa kwa ukatili
Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International
limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili
na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia
mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika
maeneo ya mpakani.
Mashambulio hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kushirikana na Israel.
Amnesty
imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa
katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu wa
Gaza,Hams inatumia fursa hiyo kujipanga kwa ushindi.BBC
Ripoti
hiyo inabainisha kuwa harakati za chama cha Hamas ambacho kimekuwa
kikiaminiwa inaonyesha kuwa imekuwa ikitumia mashambulizi ya majeshi ya
Israel kulipiza kisasi dhidi ya maadui ndani ya chama hicho.
Wapalestina
wapatao 23 kwa mjibu wa ripoti hiyo wameuawa kinyama huku mamia
wakifungwa na kuteswa, wakiwemo wanachama wa chama cha upinzani
kinachoipinga Hamas chama cha Fatah.
Hamas
imekuwa ikiwalaumu maadui zake kuwa wamekuwa wakishirikiana na Israel
ambapo ripoti hiyo inabainisha kuwa wengi ya waliouawa ni wale waliokuwa
wamefungwa gerezeni wakati wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni, ambapo
baadhi yao waliuawa kinyama hata kabla ya kesi zao kumalizika.
Katika
tukio moja la kushitua wanaume sita waliuawa kwa kupigwa risasi nje ya
Msikiti walipokuwa wamepiga magoti mbele ya umati wa watu wakiwemo
wanaume wanawake na watoto.
Ripoti
hiyo ya Amnesty inawashutumu Hamas pia kwa madai ya kupanigia haki na
uhuru kwa wapelestina wakati wao wamekuwa hawafanyi mambo yanayofanana
na yale wanayoyasema.
Shirika
la Amnesty limeitaka Hamas kushirikiana na Tume ya uchunguzi ya
kimataifa inayochunguza ukiukwaji huo wa haki za binadamu na kuwafikisha
wote waliohusika kwenye mkono wa sheria.
No comments:
Post a Comment