TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, May 19, 2015

WADAU WATAKA SERIKALI ZISIMAMIE UFUATILIAJI NA TATHMINI YA SDGs 

Sehemu ya Wawakilishi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa katika siku yao ya kwanza ya mkutano wa siku nne unaojadili juu ya mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Maendeleo Endelevu ya Maendeleo baada ya 2015. Majadiliano hayo ni moja ya eneo muhimu kueleleka ukamilishaji wa Mchakato wa Ajenda na Malengo SDGs. Mkutano huu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Afisa Mkuu wa uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla, akizungumza wakati wa Mkutano wa pembezoni ( Side-Event) ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Uwakilishi na Asasi za Kimataifa, kwaajili ya kubadilishana mawazo kuhusu nafasi za Ki Kanda na Kitaifa katika mfumo wa ufuatiliaji na udhibiti, fursa na changamoto za Malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 kwa upande wa Afrika.
Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki pamoja na mambo mengine walisisitiza haja na umuhimu wa wananchi kushirikishwa kikamilifu katika eneo hilo la ufanyaji wa tathmini na ufuatiliaji kwa kile walichosema malengo hayo ya maendeleo endelevu yanawahusu wananchi hiyo ushiriki wako ni muhimu.
Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki
Na Mwandishi Maalum,
New York
Mchakato wa ukamilishaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs) umeingia katika hatua nyingine muhimu ambapo, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana hapa makao makuu ya UM wakijadiliana kuhusu mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya malengo hayo.
Mkutano huo unaojadili aina ya mfumo wa ufuatiliaji na tathmini, utafanyika kwa siku nne na umeanza siku ya jumatatu kwa wajumbe kutoa mchango wa maoni na mawazo yao kwa kuzingatia rasimu iliyowasilishwa na wenyeviti- wenza wa mchakato wa majadiliano juu ya ajenda na malengo ya maendeleoe endelevu baada ya 2015.
Karibu wajumbe wote waliozungumza katika siku ya kwanza ya majadiliano haya, wametoa mapendekezo yao yanayotaka mfumo huo wa ufuatiliaji na tathmini uwe wa nama gani.
Akizungumza kwa niaba ya Kundi la Nchi 77 na China ( G77&China) Mwakilishi wa Afrika ya Kusini amesema nchi zinazounda kundi hilo wangependa kuona kwamba mambo yafuatayo pamoja na mengine mengi yanazingatiwa katika eneo hilo la ufuatiliaji na tathmini.
Baadhi ya mapendekezo ya G77na China ni mfumo wa ufuatiliani na tathimin uwe na upeo mpana na umilikiwe na nchi husika kwa kuzingatia mazingira yake, mahitaji yake na vipaumbele vyake.
Kundi hilo limetaka pia ufuatiliaji na tathmini, eneo ambalo ni muhimu katika utekelezaji wa SDGs lazima uongozwe na kusimamiwa na serikali na uwe wa hiari uzishikisha Wizara mbalimbali na wadau wengine ambao wataonekana kuwa ni muhimu.
Vile vile kundi la G77 na China limesisitiza haja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini unapaswa uwe ujumuishi na wenye uwiano ukizingatia pia ajenda namba 17 na malengo yote 169.
Kundi hilo la 77 na China pia limeleza kwamba ni kwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ndipo ambapo Umoja wa Mataifa utakuwa katika nafasi nzuri kutathmini utekelezaji wa ajenda za maendeleo baada ya 2015 ili kuhakikisha kwamba lengo kuu la malengo hayo ambalo ni kuondoka umaskini linafikiwa.
Wachangiaji wengine wamesisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji wa makundi yote zikiwamo Taasisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya wazugumzaji wameeleza umuhimu wa matumizi sahihi ya takwimu, uwezeshwaji katika ukusanyaji wa takwimu hizo ikiwa ni pamoja na umuhimu wa ushiriki wa Asasi zisizo za kiserikali katika mchakato huo wa ufuatiliaji na tathmini.
Wachangiaji wengine wamekwenda mbali zaidi kwa kutaka ushiriki na ujumuishi wa wananchi katika eneo hilo kwa kile wanachosema ili utekelezaji wa malengo hayo uwe wenye tija wananchi wanapashwa kuwa sehemu ya kufanya tathmini na kufuatilia kwa kuwa eneo kubwa la SDGs linahusu wananchi.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki kikamilifu katika majadiliano yote muhimu ya mchakato mzima maandalizi ya SDGs ambapo wawakilishi wa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tume ya Mipango Tanzania Bara na Visiwani na Wawakilishi kutoka Asasi zisizo za Kiserikali wamekuwa wakihudhuria mijadala hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia maslahi ya Tanzania na Bara la Afrika katika ujumla wake.
Aidha Tanzania Kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ni kiongozi wa majadiliano ( lead negotiator) kuhusu SDGs kwa Kundi la Afrika.(Muro)

No comments:

Post a Comment