Wahamiaji kujadiliwa,Malaysia
Wahamiaji huko Indonesia
Mawaziri
wa mambo ya nje wa Thailand,Malaysia na Indonesia wanafanya mkutano wa
dharula mjini Kuala Lumpur kujadili tatizo la wahamiaji haramu katika
ukanda wao.
Nchi hizo
tatu zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuwasaidia maelfu ya
wahamiaji waliokwama Baharini ambao wanahitaji chakula na maji.
Wahamiaji
wengi ni waislamu wa jamii ya Rohingya waliokimbia Myanmar, lakini
Serikali ya nchi hiyo imekataa kuhudhuria mkutano huo.
Wavuvi nchini Indonesia wamewaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano
Bado kuna
hofu kuhusu usalama wa waliokwama baharini.Maelfu ya Raia kutoka
Bangladesh na Waislamu jamii ya Rohingya wamekuwa katika bahari ya
Andaman kwa majuma kadhaa sasa.
Thailand,Malaysia na Indonesia zimekataa kuwaruhusu kuingia katika pwani za nchi zao.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment