UNICEF:Watoto zaidi wauawa Sudan Kusini
Shirika
la Umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF linasema kuwa
wavulana na wasichana wenye umri wa hadi miaka 7 wameuawa ,kutekwa na
kubakwa katika ghasia za hivi majuzi nchini Sudan Kusini.
Waathiriwa wamesema kuwa makundi yaliojihami yalichoma vijiji katika jimbo la Unity.
Mapigano
kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi yameongezeka katika majuma
ya hivi karibuni na kuwaacha zaidi ya watu laki moja bila makao.
Shirika
la msalaba mwekundu limeonya kuhusu ukosefu wa chakula huku watu zaidi
wakitoroka vita hivyo karibu na mji wa Leer wakati wa msimu huu wa
upanzi.
Vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilizuka nchini Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka
2013 baada ya rais Salva Kiir kumshtumu makamu wake Riek Machar kwa
jaribio la mapinduzi.
CHANZO:BBC......IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
No comments:
Post a Comment