TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, May 30, 2015

Muhammadu Buhari atawazwa 

Ukosefu wa usalama, rushwa, uchumi na ajira...hizo ni kama zawadi Goodluck Jonathan (kushoto) anaondoka akimuachia rais mteule wa Nigeria Muhammadu Buhari (kulia). Picha iliyopigwa Mei 28 mwaka 2015.
Ukosefu wa usalama, rushwa, uchumi na ajira...hizo ni kama zawadi Goodluck Jonathan (kushoto) anaondoka akimuachia rais mteule wa Nigeria Muhammadu Buhari (kulia). Picha iliyopigwa Mei 28 mwaka 2015.
Na RFI
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, aliyechaguliwa Aprili 1 ameapishwa jana Ijumaa katika mji mkuu Abuja. Wakati huo huo wakuu wapya wa majimbo pia wameapishwa Ijumaa wiki hii.(P.T)
Raia wengi wa Nigeria wana matumaini na Buhuri. Muhammadu Buhari alichaguliwa ili alete mabadiliko katika nyanja mbalimbali nchini Nigeria, licha ya kuwa ni vigumu kukidhi mengi miongoni mwa matarajio.
Mabadiliko ni neno muhimu, hiyo ni kauli mbiu muhimu, Muhammadu Buhari aliyokua akitumia wakati wa kampeni zake za uchaguzi. Afisa huyo wa jeshi mstaafu, ameahidi kutatua matatizo ya ukosefu wa usalama, lakini pia kukomesha umaskini na kutokomeza rushwa.
Lakini pia, timu yake imeanza kugundua, ikiwa ndio mwanzo wa kufanya kazi kwa utawala huo mpya, tatizo kubwa ambalo litawakabili ikiwa ni pamoja na mzigo wa deni la taifa ambalo ni zaidi ya dola bilioni 60, amesema Lai Mohammed, msemaji wa chama cha APC cha Muhammadu Buhari.
" Itabidi tupunguze hali ya maisha na kupitisha sheria kali za bajeti ", amesema Solomon Dalong, mjumbe wa kamati ya mpito ya kuandaa masuala ya haraka ya utawala wa Muhammadu Buhari.
Kamati hii inaamini kwamba rais mpya atafanya kazi kwa haraka kwa sababu, " miaka minne, haitoshi", amekiri mjumbe mwingine wa kamati hiyo.
Hata hivyo rais Buhari atakabiliwa na tatizo la uundwaji wa serikali na ugawaji wa nyadhifa, hasa kuwashirikisha raia kutoka majimbo ya Kaskazini Mashariki ambao walitengwa kwa kipindi kirefu na tawala ziliyotangulia ikilinganishwa na majimbo ya Kusini.

No comments:

Post a Comment