Kauli tata za Maradona kuhusu Rais wa FIFA anayewania nafasi hiyo kwa mara nyingine
Kwa sasa Rais wa FIFA Sepp Blatter hana
mpinzani baada ya wagombea wenzake wanaowania nafasi hiyo kujiondoa kwa
madai uchaguzi huo umegubikwa na rushwa zaidi badala ya haki.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika kufanyika May 26 mwishoni mwa juma hii huko jijini Zurich, Uswis.
Baadhi ya wadau wa soka duniani wamekua
na mitazamo hasi kuhusiana na Rais huyo kuendelea kuongoza Shirikisho
hilo kwa mara nyingine huku mkongwe wa soka kwa mara nyingine Maradona
akimvaa Sepp Blatter kwa kumuita kuwa ni kiongozi wa mabavu.
Kauli ya Maradona imekuja baada ya FIFA
kutengeneza mazingira mazuri ya Rais huyo kuongoza tena na kudaiwa
kuwepo mazingira ya rushwa ambayo mwenyewe ameyaita ni ya udhalilishaji.
Alisema kwa miaka ya sasa mchezo wa
mpira wa miguu umebadilika na kujaa siasa pamoja na rushwa na FIFA
wamekua wakiukandamiza kwa kuendekeza rushwa kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment