Lissu achafua hewa bungeni
Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu akizungumza bungeni wakati wa kupitisha
Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa Mwaka 2014 na Sheria wa
Makosa ya Mtandao wa Mwaka 2015 mjini Dodoma, juzi usiku. Picha na
Anthony Siame.
Dodoma.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana alichafua hali
ya hewa bungeni baada ya kudai kuwa Serikali ya Awamu ya Nne ni ya
kichovu, kauli ambayo ilizua mabishano makali kati yake na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama.
Akichangia
Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu 2015/16, Lissu alisema Serikali hiyo
imeshindwa karibu kila jambo, ikiwamo uandikishaji wa wananchi katika
Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Alisema
uchovu huo pia umejidhihirisha wazi baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kueleza kwamba mpaka sasa haijapewa fedha za maandalizi ya
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, wakati imebaki miezi mitano ufanyike.
Lissu
alivutana na Spika Anne Makinda pale alipotakiwa kukaa chini kumpisha
Mhagama azungumze baada ya kugoma kwa maelezo kuwa waziri huyo
ameingilia wakati akitoa ufafanuzi wa uchovu wa Serikali.
Mvutano
huo ulianza Lissu alipokuwa akisema kuwa mbali na kukwama kwa
uandikishaji katika Daftari la Wapigakura, hata katika upigaji wa kura
za kupitisha Katiba Inayopendekezwa katika Bunge Maalumu la Katiba,
marehemu, mahujaji na wagonjwa ni miongoni mwa wajumbe wa Bunge hilo
waliopiga kura.
"Hata
Uchaguzi Mkuu mpaka sasa Serikali haijatoa fedha kwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, hakuna maandalizi yoyote. Hatukubali kuona Serikali hii
ikijiongezea muda kwa kisingizio hicho," alisema Lissu.
Kauli
hiyo ilimwinua Mhagama na kueleza kuwa katika Bunge la Katiba zilipigwa
kura halali, huku akifafanua jinsi Serikali ilivyofanya shughuli nyingi
za maendeleo.
"Mheshimiwa
Spika, Lissu analidanganya Bunge. Kauli zake ni za kuudhi namwomba
asiendee kupotosha umma," alisema Mhagama huku Lissu akisisitiza kauli
yake.
Wakati
Mhagama akisimama kuomba utaratibu wa Spika, Lissu naye alisimama
akipinga kitengo cha kukatizwa na waziri huyo kuchangia, tukio ambalo
liliingiliwa na Spika na kuzua majibizano.
"Huyu
ananizuia kwa misingi gani, kafuata utaratibu upi," alisema Lissu huku
Mgahama naye akiendelea kuzungumza huu akiwa amesimama kabla ya wote
wawili kukatishwa na Spika Makinda aliyewataka wakae chini na kufafanua
kuwa yeye ndiye anayejua utaratibu.
Baada ya
kutoa ufafanuzi huo, Makinda alimpa nafasi Mhagama kuendelea kuzungumza
na alipomaliza alimpa nafasi Lissu ili amalizie kuchangia hotuba hiyo.CHANZO: MWANANCHI (Muro)
No comments:
Post a Comment