Vyama vipya vyatazamiwa kushiriki katika mfumo wa utawala Uhispania
Wafuasi
wa chama kipya cha Podemos washeherekea mafanikio ya chama chao katika
uchaguzi wakati wa kampeni za uchaguzi, Madrid, Mei 24.
Na RFI
Raia wa
Uhispania waliitwa Jumapili Mei 24 kuwachagua wawakilishi wao wa
manispaa na mikoa. Uchaguzi huu ni muhimu kwa nchi hiyo, ambayo imeanza
kuweka sawa mazingira yake ya kisiasa, kwa kuvishirikisha vyama vipya,
ikiwa ni pamoja na Podemos na Cuidadanos, hali ambayo inalenga kukomesha
mfumo wa utawala wa vyama viwili uliyokua ukijiri nchini humo.(P.T)
Chama cha
mrengo wa kulia kiliyo madarakani kinaongoza katika uchaguzi huo,
lakini kimepata kura zisiyoridhisha tangu kiingiye madarakani mwaka
1991.
Mazingira
ya kisiasa nchini Uhispania yamekua na motisha kufuatia uchaguzi huu wa
manispaa na mikoa. chama tawala cha PP kimeanguka kwa kiasi kikubwa
katika maeneo mengi na katika taasisi za wawakilishi katika mikoa.
Mshangao
mkubwa, kwa sasa, ni kwamba chama cha Podemos kinaweza kuongoza
Halmashauri ya jiji la Madrid, baada ya kuchukua nafasi ya pili kikiwa
karibu na chama kiliyo madarakani cha mrengo wa kulia.
Mahali
pengine, kama katika miji ya Coruna, Saragosse, Seville na Cadix,
kumeonekana kuibuka kwa vyama viwili vipya, Podemos na Ciudadanos. Chama
cha Podemos kimepata asilimia 20 za kura huku chama cha Ciudadanos
kikipata asilimia 10 za kura.
Vyama
vingine vipya vimepata kura za kutosha, na hivyo kuweka kikomo kwa mfumo
wa utawala wa vyama viwili uliyopangwa katika siasa za Uhispania tangu
kuanza kwa mfumo wa demokrasia miaka 40 iliyopita.
No comments:
Post a Comment