TPDC YAANZA UTAFITI TANGA
Mkurungezi
wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky,
akizungumza na wataalam wanao endelea na uchimbaji wa visima vifupi
katika Mradi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kwa ajili wa
utafiti wa mafuta na gesi kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani
Tanga.
Mkurungezi
wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky,
akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo
pichani) katika Mradi wa utafiti wa mafuta na gesi Ujulikanao kama MP 10
GOMBERO DRILLING PROJECT kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani
Tanga.
Meneja wa
Mradi wa MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT, Dkt. Amina Karega, akionyesha
sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kijiji
cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.
Na. Augustino Kasale - Kitengo Cha Mawasiliano-TPDC
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeanza utafiti wa mafuta na gesi eneo la Gombero, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga.
Mkurugezi
wa Utafiti kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma
Msaky, mwishoni mwa wiki alitembelea kujionea shughuli inayo fanya na
Shirika hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari alioambatana naye Dkt. Msaky alisema kuwa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeanza Mradi wa
uchorongaji wa visima vifupi kumi (10) vya utafiti wa kijiolojia wa
utafutaji mafuta na gesi katika vijiji mbalimbali mkoani Tanga
ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT.
No comments:
Post a Comment