TUME ya haki za binadamu yatoa taarifa ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu Mhe. Bahame Nyanduga akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam wakati akitoa
taarifa ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi za kuwapiga na
kuwazalilisha Viongozi na Wafuasi wa CUF huko Mtoni Mtongani Temeke, Dar
es sa Salaam.Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO
---
Na PIUS YALULA - MAELEZO
TUME ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora imelaani vitendo vya uzalilishaji
vilivyofanywa kwa Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Januari 27 mwaka
huu (2015) wakati wa maandamano ya Chama hicho Mtoni Mtongani Wilaya ya
Temeke.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo (Mei 20, 2015) Jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nanduga, alisema uchunguzi wa tukio hilo
umekamilika kwa kuzingatia kifungu cha 130[1][c],[f] na [g] cha katiba
ya jamhuri ya Aidha aliongeza kuwa sheria nyingine zilizotumika
kuchunguza tukio hilo ni pamoja na kifungu cha 6[1][c]na [g] vifungu
15[1][a] na 28[1][a],[b] na f vya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora Na.7 ya mwaka 2001, sheria ya polisi na polisi wasaidizi, sura 322,
na sheria ya vyama vya siasa, sura 258.
Nyanduga
alisema Tume yake imebaini ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu
waliofanyiwa viongozi na wanachama chama cha wananchi CUF katika
maandamano yao ya shughuli za kichama, hivyo Tume ilibaini kuwa jeshi la
polisi lilitumia nguvu kupita kiasi, ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora na udhalilishaji wa wanachama wawili wa kike wa CUF.
"Tume
imetoa mapendekezo kwa jeshi la polisi kuzingatia kanuni, sheria, haki
za binadamu na misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa majukumu
yake ya kila siku na kuhakikisha maafisa wake wanajipanga vyema katika
kuratibu na kusimamia utekelezaji wa operesheni zake" alisema Nyanduga
Kwa
mujibu wa Nyanduga tume hiyo pia imewataka Viongozi na wanachama wa CUF
kutafuta namna ya kuboresha mahusiano na jeshi la polisi, ili kuondoa
mivutano isiyo na tija.Tume imepanga kuitisha mafunzo na mikutano
mbalimbali kwa kushirikiana na vyama vya siasa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi
[NEC], pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi
na Magereza, msajili wa vyama vya siasa, na asasi za kiraia ili kupanga
taratibu zote katika kujua haki za binadamu na utawala bora.(Muro)
No comments:
Post a Comment