FAINALI YA KOMBE LA NG'OMBE ARUSHA NI ZAMZAM V/S NYOTA
Mfadhili
wa michuano ya kombe la Ng'ombe ambaye pia mkurugenzi wa kampuni ya East
Link Tanzania Ltd,Kim Fute wapili kutoka kushoto akibadilishana mawazo
na baadhi ya vijana waliofika kushuhudia michuano hiyo ,michuano hiyo
itahitimishwa mapema siku ya jumapili wiki hiii katika uwanja wa shule
ya msingi Sinoni ambapo Timu ya Zamzam na Nyota watachuana.
Taswira ya muonekano wa mlima Meru unavyoonekana pichani,hii ilikuwa juzi katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.
Baadhi ya
wachezaji wa klabu ya Zamzam FC wakimwangalia mlinda mlango wao
,Seleman Casillas mara baada ya kuanguka na kulalamika kuua mguuni juzi
katika mechi baina yao na Parrot katika kombe la Ng"ombe iliyochezwa
katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha,klabu ya Zamzam
ilifanikiwa kutinga fainali katika mchezo huo ambapo itakutana na Nyota
siku ya jumapili
Soka ni
mchezo wa ajabu embu sikia hii mlango wa klabu ya Parot FC,Sacrifice
Adam juzi alijikuta akiangua kilio uwanjani mara baada ya kushuhudiwa
timu yake ikitolewa katika michuano ya kombe la ng'ombe linaloendelea
kuwaka moto katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha.
Adam,aliangua
kilio wakati alipokuwa akishuhudia timu yake ikiondolewa na klabu ya
Zamzam FC juzi katika viwanja hivyo katika hatua ya matuta baada ya timu
yake kuchapwa kwa jumla ya penati 5 kwa 4.
Hatahivyo,hapo
awali Adam alifanikiwa kuokoa mipira mingi ya hatari iliyokuwa ikipigwa
na washambuliaji wa klabu ya Zamzam hususani wakati timu hizom
zinakkwenda kumalizia kipindi cha pili.
Kwa hatua
hiyo klabu ya Zamzam sasa imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia katika
hatua ya fainali ambapo itakutana na Nyota siku ya kesho (jumapili)
katika viwanja hivyo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mdau wa michezo
jijini Arusha na mkurugenzi wa kampuni ya East Link Tanzania Ltd,Kim
Fute.(V.S)
No comments:
Post a Comment