Michuano ya COSAFA yaanza Africa Kusini
Michuano ya COSAFA,nchini Afrika Kusini
Michuano
ya kumi na tano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu kusini mwa
Afrika,COSAFA imezikutanisha timu za ukanda huo nchini Afrika Kusini.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Jumapili mei 17 na itakamilika mei
30
Timu 12
kati ya 14 kutoka nchi wanachama wa COSAFA tayari zipo nchini Afrika
Kusini kuchuana katika mashindano hayo. Angola na Comoro ambazo ni
wanachama wa COSAFA hazikuweza kushiriki mwaka huu.
Nafasi
zao zimechukuliwa na Ghana iliyofikia fainali za michuano ya Caf ya
mwaka huu na Tanzania kutoka ukanda wa Afrika mashariki na kati ikiwa
mwanachama wa CECAFA.
Timu nane
zenye viwango vya chini kwa ubora kwa mujibu wa takwimu za FIFA kwa
mwezi Februari, zimepangwa katika makundi mawili yenye timu nne kila
moja, Tanzania ikiwemo katika michuano hiyo.
Kundi A
lina timu za Zimbabwe, Namibia, Seychelles na Mauritius. Ambapo kundi B
lina timu za Madagascar, Lesotho, Swaziland na Tanzania.
Katika
kundi A Zimbabwe inaoongoza kundi hilo kwa kujikusanyia pointi sita
baada ya michezo miwili ikifuatiwa na Namibia yenye pointi nne.
Seychelles ni ya tatu na pointi moja. Mkiani ni Mauritius ambayo haina
pointi.
Na katika kundi B, Madagascar na Swaziland zote zina pointi tatu, huku Lesotho na Tanzania zikiwa mikono mitupu.
Tanzania
leo,Jumatano inarusha karata yake ya pili kwa kupambana na Madagascar
baada ya kucharazwa bao 1-0 na Swaziland katika mchezo wake wa kwanza.
Timu za
juu katika kila kundi zitasonga mbele hatua ya mtoano, ambapo timu sita
za viwango vya juu zitaingia katika mashindano hayo yakiwa katika hatua
ya robo fainali na kuendelea. Afrika Kusini kutokana na ubora wake
itapambana na Botswana hatua ya robo fainali.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment