TUZO YA BBC:HEKO KWA ASISAT OSHOALA
Mshambuliaji
wa Nigeria na timu ya Wanawake ya Liverpool, Asisat Oshoala ametangazwa
kuwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa mwaka.
Oshoala,
mwenye umri wa miaka 20 ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo mpya kutoka
BBC World Service,kwa kura zilizopigwa na wapenzi wa kandanda duniani.
Mwanadada huyu amemuangusha Veronica Boquete wa Uhispania na Nadine Kessler wa Ujerumani,Scot Kim Little na Marta wa Brazil.
"ninapenda kutoa shukrani zangu kwa BBC,mashabiki wangu duniani na kila mmoja aliyepiga kura" alisema.
Tuzo hii ni ya kwanza kufanyika na Shirika la utangazaji la kimataifa.
Oshoala,
ambaye ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wapinzani wake,
alikuwa mfungaji bora na alipigiwa kura wakati wa michuano ya kombe la
dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20 nchini Canada kipindi
cha majira ya joto kilichopita.
Jitihada
zake ziliifikisha Nigeria katika hatua ya Fainali ambapo ilikutana na
Ujerumani, ambapo Ujerumani ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Nigeria.
Pia
alitoa mchango mkubwa katika timu ya wanawake ya Nigeria katika kutwaa
ushindi wa kombe la mabingwa Afrika kwa wanawake mwezi Oktoba.
Hatua
hiyo imeiwezesha Nigeria kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa
wanawake nchini Canada inayoanza tarehe 6 mwezi Juni
CHANZO:BBC
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
No comments:
Post a Comment