Mtu mmoja auawa katika machafuko mapya Bujumbura
Na RFI
Hali ya
usalama imeendelea kudoroara nchini Burundi, hasa katika mji wa
Bujumbura. Raia mjini humo wameendelea kushikilia msimamo wao wa
kuandamana hadi rais Pierre Nkurunziza atakapo achana na mpango wake wa
kuwania muhula wa tatu.
Maandamano
yameingia Jumanne Mei 12 katika siku yake ya kumi na tano mjini
Bujumbura, ambapo wanawake na wasichana wameonekana katika mstari wa
mbele katika maadamano hayo.
Zaidi ya
wanawake na wasichana wameandamana katika wilaya ya Musaga, kusini mwa
jiji la Biujumbura. Maandamano hayo ya wanawake na wasichana yamefanyika
siku mbili baada ya maandamano mengine ya wanawake na wasichana wasomi
yaliyofanyika mjini kati Bujumbura Jumapili mwishoni mwa juma hili
lililopita.(P.T)
Wanawake
na wasichana wa wilayani Musaga wameapa kuendelea na maadamano. Uamzi
huo wa wanawake na wasichana wa kuandamana umekaribishwa na waandamanaji
walioanza maandamano hayo.
Mtu mmoja aauawa kwa kupigwa risasi wilayani Buterere
Wilayani
Buterere, kaskazini magharibi mwa jiji la Bujumbura, maandamano
yameendelea. Katika maandamano hayo wameonekana pia wanawake na
wasichana. Wakati huo huo polisi ilijitahidi kuwatawanya waandamanaji.
Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi mapema Jumanne
asubuhi wiki hii.
Kutokana
na hali hiyo waandamanaji wamepandwa na ghadhabu na kuamua kuchoma moto
ofisi mbili za chama tawala cha Cndd-Fdd, na baadaye walijaribu
kushambulia nyumba ya afisa wa polisi anayejulikana kwa jina maarufu
Ayubu, ambaye amekua akituhumiwa na waandamanaji kuwa amekua
akijihusisha na vitendo vya kikatili dhidi ya waandamanaji. Wakati huo
huo gari ndogo la mkuu wa wilaya ya Buterere limechomwa moto na
waandamanaji wenye hasira.
Duru
kutoka shirika la msalaba mwekundu, zaidi ya watu 150 wamejeruhiwa
kataika maandamano hayo, na wamelazwa katika hospitali mbalimbali za mji
wa Bujumbura.
Hayo
yanajiri wakati viongozi mbalimbali kutoka Umoja wa Afrika wakiwemo
marais wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Kati wakitazamiwa
kukutana jijini Dar es Salaam kwa minajili ya kutafutia suluhu machafuko
yanayoendelea nchini Burundi.
Rais
Nkurunziza ameendelea na msimamo wake wa kuwania muhula wa tatu, baada
ya viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa
Ulaya, Umoja wa Afrika, Marekani na mataifa jirani kumnasihi rais huyo
kujiondoa katika kinyanga'nyiro hicho cha kuwania urais.
No comments:
Post a Comment