Kipaji kinalipa… hapa kuna picha ya Mbwana Samatta na gari lake jipya.
Samatta
anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji watanzania wanaoingiza fedha
nyingi kupitia soka – akiripotiwa kulipwa mshahara usiopungua $8000 kwa
mwezi bila kuongeza marupurupu.
Mmoja ya wachezaji wa kitanzania wenye mafanikio katika soka nje ya
mipaka ya Tanzania, Mbwana Samatta leo asubuhi ameposti picha ya gari
lake jipya analotumia akiwa nchini Tanzania.
Gari
aliloposti Samatta ni Range Rover lenye rangi ya damu ya mzee ambalo
lina namba za usajili za Tanzania na linakua gari la pili la thamani
ambalo Samatta ameliweka hadharani baada ya mwaka 2013 kulionyesha gari
lake aina ya Chrysler Crossfire ambalo lilikuwa na thamani ya takribani
millioni 50 za kitanzania.
Samatta alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba SC kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa kipindi hicho ya $100,000.
No comments:
Post a Comment