MARAIS AFRIKA MASHARIKI WALAANI JARIBIO LA KUPINDULIWA NKURUNZINZA
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam.
Na Chalila Kibuda
MARAIS wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki wamelaani kitendo cha baadhi ya askari
kufanya jaribio la kutaka kuipindua serikali ya Burundi.
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amesema kuwa hali ya
Burundi ni tete na kwamba japo linaonekana ni jambo dogo lakini linaweza
kugharimu maisha ya watu.
"Hivyo
tunatakiwa tuvute subira...Tusubiri na sio kulitangaza suala hilo
kiushabiki wakati wenzetu wana tatizo. Afrika haitaki tena mtu yeyote
kwa sababu yeyote kuhalalisha kuchukua nchi kwa mtutu", amesema Membe.
Amesema
Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo lilikuwa na
mkutano juzi na jana, litakaa tena wiki ijayo kujadili ajili ya hali ya
Burundi.
Membe
amesema, Wakuu hao wataketi tena Jumatatu baada ya kupata tathimini na
watatoa taarifa ya kinachoendelea nchini Burundi, hivyo kwa sasa
hawatazungumzia lolote.
Membe
amesema kuwa hajui aliko Rais Pierre Nkurunzinza ambaye anadaiwa
aliondoka nchini jana kurudi Burundi huku kukiwa na taarifa za kutokwepo
kwa Rais huyo katika nchi yake kufuatia jaribio la kupinduliwa na
baadhi wa askari wa nchi hiyo.(Muro)
No comments:
Post a Comment