Sentensi tisa za Nape Nnauye kuhusu ishu ya Mwigulu Nchemba kuomba kujivua nafasi yake ndani ya CCM !!
Naibu Waziri wa Fedha, Lameck Mwigulu Nchemba
jana jina lake liliingia kwenye headlines baada ya kutangaza kujivua
kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.. hiyo ishu
ilichukua nafasi kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii kuanzia siku ya
jana May 24 2015, leo anayeingia kwenye headlines ni Nape Nnauye, Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM amezungumzia kuhusu ishu ya Mwigulu Nchemba alivyojitoa kwenye nafasi yake hiyo ndani ya Chama.
“Tumejadili mambo mengi nikaona hili moja nilitoe mengine tutaendelea kupeana” Nape Nnauye.
“Mwishoni mwa kikao Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara ndugu Lameck Mwigulu Nchemba
ameomba kwa Halmashauri kuu ya Taifa kupumzika kwa sababu ya nia yake
ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa nafasi ya Urais”Nape Nnauye.
“Ametumia busara na wajumbe wameridhika, wamepongeza busara yake”
“Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa akamteua Rajabu Luhavi
kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ikampitisha
kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Tanzania bara.. amekuwa msaidizi wa
Rais Ikulu mambo ya siasa sasa anahamia kwenye chama” Nape Nnauye.
Kama unataka kuisikiliza sauti ya Nape Nnauye unaweza kuplay hapa umsikie akimzungumzia Mwigulu Nchemba.
No comments:
Post a Comment