Brendan Rodgers kuihama Liverpool?
Kipigo cha aibu walichokipata Liverpool dhidi Stoke City jana kimepelekea kocha wao Brendan Rodgers kutamka maneno mazito juu ya hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Kocha huyo amesema yupo tayari kuondoka endapo wamiliki wa klabu hiyo watamtaka kufanya hivyo.
Liverpool
imejikuta ikiaibishwa kwa kipigo cha magoli 6-1 kutoka kwa Stoke City
ikiwa ni mchezo wa kufungua pazia la ligi kuu ya England jana pamoja na
mechi ya mwisho wa nahodha wao Steven Gerrard.
Hata
hivyo amesema anasikitishwa na matokeo ya jana ya timu hiyo kufungwa
magoli sita na kusema wamedhalilika kwani kwa miaka miangi hawajawi
kufungwa idadi kubwa kama hiyo ya magoli na amesisitiza mashabiki
wanaitaji kuomba radhi.
No comments:
Post a Comment