EU kupambana na wahamiaji haramu
Wahamiaji wakiwa wameketi katika kituo kimoja mjini Tripoli wakiwa na matumaini ya kufika Ulaya
Umoja wa
ulaya umekubali kuanzisha kikosi cha Jeshi la wanamaji kwa ajili ya
kupambana na wafanya biashara wanaosafirisha watu kutoka Libya.
Mkuu wa
sera za mambo ya kigeni wa EU,Federica Mogherini, amesema nia ni kuvunja
mtandao unaowasafirisha wahamiaji kupitia bahari ya Mediterania.
Mogherini amesema umoja wa ulaya utaendelea kutafuta kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhusu kikosi hicho kipya.
Lakini
Serikali ya Libya inayotambulika na jumuia ya kimataifa imesisitiza kuwa
itahitaji kushirikishwa katika kuratibu operesheni za kijeshi dhidi ya
wahalifu hao.
Balozi wa
Libya ndani ya Umoja wa Mataifa, Ibrahim Dabbashi, amesema Mamlaka za
libya hazijaelezwa chochote kuhusu Operesheni hiyo kwenye milki yake.
Dabbash
amesema mipango ya EU pekee haiwezi kumaliza tatizo la wahamiaji haramu
isipokuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuisaidia Serikali halali ya Libya
kuweza kudhibiti mipaka yake hali itakayorahisisha kukomesha wimbi la
wahamiaji haramu.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment