MKUU WA MKOA WA NJOMBE AFUNGUA KIKAO KAZI CHA BIASHARA YA KILIMO
Mkuu wa
Mkoa wa Njombe, Mh. Dk. Rehema Nchimbi akifungua kikao kazi cha biashara
ya kilimo kwa kongani ya Ihemi iliyoandaliwa na SAGCOT (Southern
Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kwa ushirikiano na UONGOZI
Institute (Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu) mapema leo
Iringa mjini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kilimo wa
TCCIA Bi. Magadalena Mkocha, Mwenyikiti wa Bodi ya Agricultural Council
of Tanzania Dk. Sinare Y. Sinare, DC wa Iringa Mh. Angeline Mabula, DC
wa Mufindi Mh. Mboni Mhita na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon
Luhanjo.
Katibu
Mkuu Kiongozi mstaafu, Philemon Luhanjo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti
wa bodi ya UONGOZI Institute akitoa salaam kwa niaba ya taasisi hiyo
wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya
Ihemi inayoendelea Iringa mjini. UONGOZI Institute imeshiriki katika
kuwezesha kikao kazi hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa SAGCOT, Bw. Geoffrey Kirenga akitoa utangulizi wa mada ya
biashara ya kilimo kwa nyanda za juu kusini. Mkutano huu wa siku mbili
unakutanisha viongozi wa serikalini, sekta binafsi, mashirika ya
kimataifa pamoja na wakulima kwa ajili ya kujadili kuhusu kuboresha
biashara ya kilimo nchini kwa nyanda za juu kusini.
Picha ya
pamoja ya wageni waalikwa na washiriki wa kikao kazi cha biashara ya
kilimo inayoendelea Iringa mjini. Mada zinazojadiliwa ni pamoja na
wajibu wa viongozi katika kuleta mageuzi katika kilimo.(Muro)
No comments:
Post a Comment