Madagascar : wabunge wapiga kura ya kujiuzulu kwa rais
Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, Januari mwaka 2014.
Na RFI
Mvutano
wa kisiasa umejitokeza nchini Madagascar. Wabunge 121 kwa jumla ya
wabunge 125 walioshiriki kikao cha Bunge Jumanne wiki hii, wamepiga kura
ya kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina, mwaka
mmoja na nusu baada ya kuchaguliwa kwake kuliongoza taifa hilo.
Wabunge
hao wanamtuhumu rais Hery Rajaonarimampianina kwamba amekiuka katiba ya
nchi. Rais huyo anaonekana kupoteza imani kwa wabunge hao.
" Hajui
majukumu yake, hawezi kuliongoza taifa la Madagascar ", wamesema baadhi
ya wabunge. Tuhuma hizo dhidi ya rais Hery Rajaonarimampianina zimeibuka
katika kikao cha Bunge cha Jumanne jioni wiki hii, ambapo kikao hicho
kiligubikwa na mvutano. Baada ya kikao, baadhi ya wabunge walitaka
kuzipiga, na hali hiyo ikapelekea wanajeshi wanaolinda jengo la Bunge
kuingilia kati ili kuzuia rabsha isitokei.(P.T)
Wakiwa na
hasira, wabunge hao wamemkosoa rais kwamba hana uamzi katika majukumu
yake. Ilimpasa zaidi ya miezi miwili ili kupata waziri mkuu, kabla ya
kumfuta kazi baada ya miezi minane. Mahakama Kuu ambayo ingeliundwa
katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa rais haijaundwa.
Herry Rajaonarimampianina pia anatuhumiwa kujaribu kushawishi kazi ya
wabunge.
Kazi kubwa kwa Mahakama Kuu ya Katiba
Lakini
hasira za wabunge zililipuka baada vikao vya kuboresha Maridhiano,
vilivyohitimishwa wiki tatu zilizopita. Hakuna mbunge aliyealikwa
miongoni mwa washiriki 2,000 waliohudhuria vikao hivyo. Na kuvunjwa kwa
Bunge ilikuwa miongoni mwa mapendekezo ya mwisho ya vikao hivyo. Kura
iliyopigwa Jumanne wiki hii ina kinga fulani kwa wabunge.
Mahakama
ya Katiba (HCC) na majaji wake tisa ndio wana majukumu ya kuthibitishwa
au la kwa kujiuzulu katika siku zijazo kwa rais huyo.
Herry
Rajaonarimampianina bado ni rais mpaka pale uamzi wa Mahakama ya Katiba
wa kujiuzulu kwa rais huyo utatolewa. Inasemekana kuwa majaji wa
Mahakama ya Katiba ni washirika wa karibu wa utawala.
No comments:
Post a Comment