Unicef : Dola za Marekani Milioni 500 zahitajika Iraq
Mpiganaji wa Islamic State akibebelea bendera ya kundi lake, karibu na mpaka wa Iraq na Syria.
Na RFI
Mashirika
mbalibali ya kibinadamu yanapanga kuzindua mchango wa kutafuta Dola za
Marekani Milioni 500 kukabiliana na hasara iliyosabishwa na wapiganaji
wa Islamic State nchini Iraq.
Mchango huu unasimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto Unicef.
Mwakilishi
wa Unicef nchini Iraq Philippe Heffinck, amesema hali ya kibainadamu
nchini humo ni mbaya sana na shirika hilo linahitaji fedha hizo ili
kuendelea kuwasaidia zaidi ya watu Milioni 8 waliothirika.
Haya
yanajiri wakati huu Marekania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa
kimataifa jijini Paris nchini Ufaransa kujadili namna ya kuendeleka
kukabiliana na Islamic State nchini Iraq na Syria.(P.T)
No comments:
Post a Comment