TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, June 2, 2015

Baba amfungia mkewe bafuni kwa miaka mitatu kisa mtoto wa kike…unajua alikua anampa nini?

man
Suala la kuchagua jinsia ya watoto ni makubaliano kati ya wazazi na pia huwahusisha wote wawili, lakini pia ujio wa mtoto mwenye jinsia yoyote ndani ya familia ni mapenzi na baraka za Mungu
Mwanaume huyu raia wa India hakupishana na baadhi ya wanaume wengi ndani ya jamii zetu ambao wamekua na chaguo lao wenyewe pindi linapokuja suala la kupata mtoto.
Rameshwar Rao aliamua kumfungia mkewe na mtoto wake wa kike bafuni kwa muda wa miaka mitatu kisa tu amemzalia mtoto wa kike kinyume na matarajio yake ya kupata mtoto wa kiume.
Baada ya mkewe Priyanka kugundua ni mjamzito wa mtoto wa kike alimwambia mumewe ambaye alimtaka aitoe mimba kwa kuwa alitaka mtoto wa kiume, lakini mkewe alikataa kuitoa na kuamua kurudi kwa wazazi wake akajifungue.
Alikaa kwa wazazi wake takribani miaka mitano na kuamua kurudi wakati mtoto akiwa tayari mkubwa baada ya wote kusameheana, lakini cha kushangaza mwanaume aliamua kuwafungia bafuni yeye na mtoto wake huku akiwapa maji na wali kwa muda wote.
Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa na polisi baada ya marafiki wa familia yake kugundua kitendo alichokifanya kwa mkewe lakini mke wake amewaomba polisi hao kumwachia huru ili waendelee kuishi pamoja

No comments:

Post a Comment