AC Milan na Inter zavunja rekodi ya miaka 60 michuano ya Ulaya
Wakati fainali ya Champions League kwa mwaka 2016 ilipotangazwa itachezwa katika dimba la San Siro, mashabiki wa vilabu vya AC Milan na Inter Milan vinavyotumia uwanja huo kwa mechi walianza kuwa na ndoto za kupata ufalme wa soka barani Ulaya katika uwanja wao wa nyumbani.
Ni Real Madrid pekee ambao wameshinda ubingwa wa Ulaya mara nyingi kuliko AC Milan, wakati miaka 5 iliyopita Inter Milan walitwaa ubingwa huo.
Lakini wakati vigogo viwili vya soka barani Ulaya vitakuwa vikiutafuta ubingwa wa Ulaya jijini Milan Mei 2016, hakutakuwa na nafasi ya wenyeji wa mji huo kupata uwakilishi kwenye michuano hiyo.
Timu hizo mbili pia hazitopata hata nafasi kushiriki kwenye michuano midogo ya Europa, hii ni rekodi ya ambayo haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 60 kwa AC Milan au Inter kushindwa kucheza katika michuano ya Ulaya.
Vilabu hivyo vimeshindwa kumaliza katika nafasi 5 za juu za ligi ya Serie A na hivyo kushindwa kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya Ulaya.
Inter Milan imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 8, huku AC Milan ikiwa nafasi ya 10.
No comments:
Post a Comment