SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO WATAKIWA KUFUATA HAKI ZA BINADAMU
Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali
na wadau wa maendeleo wametakiwa kuzingatia usawa,haki,sheria
ilikutimiza wajibu wao wa kutoa huduma kwa jamii yenye ulemavu wa ngozi
sawa na kufuata haki za binadamu ili kufikia malengo ya milenia.
Kauli
hiyo imetolewa na mkurugenzi mkazi wa umoja wa mataifa hapa nchini
Alvaro Rodrigues wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya kilele cha
siku ya walemavu duniani yaliofanyika kitaifa mkoani hapa.
Rodrigues
alisema kuwa tunaposherehekea siku hiyo ya kupata ufahamu juu ya watu
wa jamii yenye ulemavu wa ngozi(ALBINO)tunawaji kujua kuwa jamii hiyo
inahitaji nini na je mahitaji yao yanapatikana ikiwemo kupewa ulinzi wa
maisha yao kama usawa,haki na sheria.
Alisema
kuwa Angependa kuzungumzia mambo makubwa matatu yatakayo wakumbusha
jamii kwa kuwa ni kweli kuna maendeleo katika kuboresha haki za binadamu
hapa nchini katika makundi yote hivyo umoja huo ulikishirikiana na
serikali na wadau wa maendeleo utambue wajibu wao kwa watu wa jamii hiyo
kwani hiyo ni moja kati ya haki za binadamu.
Aidha
aliwataka kufanyaikazi kwa nia ya dhati na kuzuia na kukomesha ukatili
dhidi yao kwa watu wenye ulemavu wa ngozi bila kusahau kuwa watu wa
jamii hiyo wamekuwa hawana uwezo wa kumudu gharama mbalimbali zikiwemo
dawa,hivyo wapewe kipaumbele kwani ni haki yao ya kimsingi.
“Umoja wa
mataifa unaendelea kufanyakazi kwa pamoja na serikali na jamiii kwa
ujumla kuboresha utawala wa sheria katika kila mwelekeo pamoja na watu
wenye ulemavu wa ngozi hapa lazima tuipongeze serikali kwa kufuatilia
kwa ukaribu mauaji ya jamii hii ila tuwapende tuwatunze kwani binadamu
waote ni sawa”alisema Rodrigues
Nao
jumuiya ya ulaya katika taarifa yao kwa vyombo vya habari wamaepinga
mauaji ya jamii hiyo na kuitaka serikali kuchukua hatua stahiki
kuwalinda na kuheshimu haki za binadamu kwa kuwapatia mahitaji stahiki
jamii hiyo kwani imekuwa inakumbana na changamoto kubwa katika maisha
yao ya kila siku.
Kwa
upande wake raisi wa taasisi ya social Protection Association Hassan
Abdulrahman alisema kuwa wao wameandaa Bonanza la kupinga mauaji ya
albino litakalofanyika jijini Dar es salaam sanjari na kongamano kwa
wanafunzi wa vyuo 10 mkoani humu.
Alisema
kuwa hiyo yote ni katika kuahakikisha masuala ya mauaji ya watu wenye
ulemavu hapa nchi yanakuwa historian a watu wanajali haki za binadamu
wenzao kwani ukatili huo unatisha na unawanyima haki yao ya kuishi.
Alisema
wanatarajia kwa kila chuo kuwafikia wanafnzi zaidi ya mia mbili na
baadae kutoa elimu kwa jamii ya watanzania wote kufahamu madhila
wanayopata wenzao katika maisha yaoa ya kila siku na kuwa bonanza na
kongamano vitafanyika mwishoni mwa mwezi huo na mwezi ujao.
Wakati
huo huo umoaj wa waganga wa jadi hapa nchi umepinga vikali sula la
upigaji ramli kwa waganga wa jadi katika kuhakikisha dhana potofu ya
kuwa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi vinaleta utajiri.
Akizungumza
na gazeti hili Mratibu wa umoja huo Julius Juju alisema kuwa changamoto
kubwa wanayokumbana nao kwenye majukumu ya kazi yao ni upigaji wa ramli
nah ii ndiyo sababu kubwa inayopelekea mauji hayo nao wanayapinga kwa
nguvu zao na kuwa watashirikiana na serikali kwa ukaribu kuhakikisha
wale wote wenye dhna potofu wanaingia kwenye mikono ya serikali.
Akatanabaisha
kuwa wamekuwa wakipata changamoto kutoka kwa waratibu wa afya wa
serikali ambao wamekuwa wakichelewesha ushirikiano wao na serikali
katika kufikia malengo na kuondoa tatizo wao wanapinga mauaji hayo
wakiamini viungo vya Albino haviwezi kuwapatia wananchi utajiri.
“Hapa
ikumbukwe kuwa kutetea hai za binadamu wengi sanjari na uedeshaji wa
kupiga ramli ndio changamoto kubwa katika mauaji ya jamii sisi kama
uwawa tunapinga mauaji na tunapenda kutambulika kisheria katika serikali
yetu na tutatoa ushirikiano kuhakikisha wenzetu wachache wanaotuchafua
sheria inachukuwa mkondo wake”alisisitiza Juju.(Muro)
No comments:
Post a Comment