Mama Tunu Pinda azindua Taasisi ya Manjano Foundation
Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama
Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha
Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa
Mengine.
Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania
mama Tunu Pinda. Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch
Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na
walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya
bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote
na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa
za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa
hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.
Mtoa
Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo
kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha
Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza
Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila
pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata
Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .
Hafla
hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo
imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo
zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na
ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha
yake.
Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari
ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha
LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear
illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa
kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na
vipodozi sahihi. (DK)
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati
akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia)
Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar.
Balozi
wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya
Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv Touch.
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) akiwa na mtoa mada katika halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch
Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation.
Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bondo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Pili
Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda wa
Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi
Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
wageni walikwa
No comments:
Post a Comment