Miili 23 ya ajali ya basi la Another G na lori Mufindi Iringa yatambuliwa
Mkuu wa
wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita (kushoto) akiwa na
wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo ya Mufindi katika
kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi.
Baadhi ya ndugu wakichukua mwili wa ndugu yao baada ya kuutambua
Mkuu wa
wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto) akimfariji mmoja kati ya
majeruhi wa ajali ya basi la Another G na lori iliyoua 23 na kujeruhi
34 jana, wengine pichani ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
wilaya ya Mufindi (picha na matukiodaimaBlog).(DK)
*DC Mhita awashauri TBS kukagua ubora wa vyombo vya usafiri
MIILI
yote 23 ya ajali ya basi aina Coaster mali ya kampuni ya Another G
lenye namba za usajili T 927 CEF aina ya mitsubishi fuso iliyokuw3a
ikifanya safari zake kati ya Iringa – Njombe ambalo liligoganga na
uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T 916AQM likiwa na Tela
lenye namba za usajili T 965 BEH Scania imetambuliwa na ndugu zao.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Mufindi ambae ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya Bi Mboni Mhita kuwa ndugu wa marehemu hao
waliokufa katika ajali waliweza kutambua miili ya ndugu zao jana na
leo na kuwa hadi sasa hakuna mwili ambao bado kutambulia na hivyo
kuvishukuru vyombo vya habari kwa kushiriki kuhabarisha juu ya ajali
hiyo na wananchi ambao waliitikia na kufika kutambua miili hiyo.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz Mkuu huyo wa wilaya Bi
Mboni alisema kuwa jitihada kubwa zimeonyeshwa na vyombo vya
habari vya ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa ikiwemo mitandao
ya kijamii katika kuhabarisha umma na ndio sababu ya utambuzi wa
miili hiyo kufanikiwa mapema baada ya habari kuenezwa vilivyo.
Pia
mkuu huyo wa wilaya alipongeza uongozi wa JKT Mafinga na uongozi
wa kitaifa wa jeshi hilo kwa kujitolea kusaidia mazishi ya vijana
wake ambao walikuwa wakielekea JKT Mafinga kwa ajili ya kuripoti kwa
kuanza mafunzo ya jeshi na baadhi yao kufa katika ajali hiyo huku
baadhi wakijeruhiwa kwani alisema ni vigumu kwa taasisi kujitolea
kusaidia mtu ambae hana mkataba nae.
Aidha
mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wananchi wote nchini ambao ndugu zao
walipoteza maisha katika ajali ya basi la Majinja lililoua watu zaidi
ya 50 katika eneo la Changalawe mjini Mafinga kufika kituo cha
polisi Mafinga kwa ajili ya kutambua na kuchukua mizigo ya ndugu zao
waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwa mali zote za marehemu hao
zimehifadhiwa salama.
Hata
hivyo mkuu huyo wa wilaya ya Mufindi Bi Mboni alivitaka vyombo vya
usalama barabarani katika wilaya ya Mufindi kuendelea na mkakati
wake wa kuwabana madereva wanaovunja sheria za barabarani na
kuwachukulia hatu kali kama njia ya kupunguza ajali hiyo.
Alisema
askari hao pia wanapaswa kukagua ubora wa vyombo vya usafiri
vyote na vile ambavyo havina ubora ni heri kuvifungia hadi
vitakapoboreshwa kuliko kuruhusu vyombo vya usafiri chakavu
kufanya kazi ya usafirishaji wa abiria .
Kuhusiana
na wajibu wa shirika la viwango Tanzania (TBS) mkuu huyo wa wilaya
alishauri kuwepo na mkakati makini wa TBS kukagua ubora wa vyombo
vya usafiri vinavyoingizwa nchini kwani mabasi mengi ya abiria siti
zake zimeshikiliwa na ngundi ya mbao na baada ya kutokea ajali siti hizo
hung’ooka na kama abiria amefunga mkanda hulazimika kuchomoka na siti
yake .
Alisema
katika ripoti ya ajali ya kwanza ya basi la Majinja iliyotokea Machi
mwaka huu na kuua watu zaidi ya 50 kamati ya uchunguzi ilibainihilona
kuwa mwenye uwezo wa kukagua viwango vya vyombo hivyo vya usafiri ni
TBS kwa kushirikiana na wadau wengine kama Sumatra na jeshi la polisi
kupitia kitengo cha usalama barabarani.
Wakati
serikali ya wilaya ya Mufindi kupitia mkuu huyo wa wilaya ikishauri
TBS na washirika wake kuweka mkakati wa kukagua viwango vya
vyombo hivyo vya usafiri baadhi ya wananchi wilaya ya Mufindi na
mkoa wa Iringa wamekuwa na maoni tofauti kwa kulitaka jeshi la polisi
kitendo cha askari wa usalama barabarani kuanza kusindikiza mabasi hayo
yanayotoka usiku mkoani Njombe na Iringa ili kuhakikisha abiria
hawazidi katika mabasi hayo ya usiku.
Zacharia
Sanga mkazi wa Mafinga wilaya ya Mufindi na John Lumwesa mkazi wa
Iringa mjini walisema kuwa kimsingi mabasi hayo yanajaza abiria
kupita kiasi na kutembea kwa mwendo mkali zaidi kutokana na nyakati za
usiku askari wa usalama barabara kutokuwepo.
Hivyo
walitaka askari wa usalama barabarani kuendelea kuwepo na tochi hadi
usiku ili kuthibiti ajali mbaya kama hiyo ambayo mbali ya kuwa ni
uzembe wa dereva wa basi ila kukosekana kwa askari wa usalama
barabarani usiku ni moja ya sababu.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Mufindi Dr Godluck Mlimbila alisema
kuwa hali za majeruhi 34 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali hiyo
zinaendelea vizuri na kuwa mbali ya wale wanne ambao hali zao
zilikuwa mbaya zaidi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa katika Hospitali hiyo hadi jana majira ya saa 8 mchana ni
majeruhi kati ya 8 na 10 pekee ndio ambao walikuwa wakiendelea na
matibabu huku wengi wao wakiwa wameruhusiwa baada ya hali zao
kuendelea vema .
No comments:
Post a Comment