Lori la mafuta lawaua watu 70 Nigeria
Lori la mafuta lawaua watu 70 Nigeria
Karibu watu 70 wamefariki huko mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto.
Police wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali.
Walioshuhudia
wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti ndiposa likakosa
mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri
usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.
Mmoja ya waliokuwa wakishughulika kuwanusuru waliojeruhiwa amesema magari mengine 12 nayo yalishika moto.
Mwandishi wa BBC aliyeko Nigeria anasema mikasa ya ajali zinazohusu magari ya kubeba mafuta hutokea mara kwa mara nchini humo.
Miaka
mitatu iliyopita ajali mbaya sana ya moto wa mafuta iliwaua zaidi ya
watu 100 huko Niger Delta katika mkasa uliochangiwa na watu kuchota
mafuta yaliomwagika baada ya gari kubwa la mafuta kupata ajali.BBC
No comments:
Post a Comment