DJ Khaled kumbe anaogopa kusafiri kwa ndege !! Kisa ni hiki alichosema hapa..

Producer, Rapper na DJ wa muziki Marekani, Dj Khaled siku chache zilizopita alikuwa kwenye Interview moja ya Radio ndani ya Los Angeles, Marekani.
Kati ya mambo waliyoongelea kuna kitu kimoja nimekijua baada ya kumsikia kwenye Interview hiyo… DJ Khaled aliulizwa kwa nini hapendi kutumia usafiri wa ndege>>>“…aah
 bwana mimi ndege zinanipa presha, sio utani, pale ndege inapoanza 
kuondoka uwanjani kuna ule muungurumo na mtikisiko wa ndege inapoanza 
kupaa… ile mimi inanipa tumbo joto yani hua napanic, natoa jasho 
natetemeka na vitu kama hivyo yani!! kibaya zaidi unakuta Pilot wa ndege
 anatoa tangazo kua hali ya hewa itakua mbaya safari nzima! Hapo 
inamaanisha safari nzima tutakua tumeshikilia roho zetu mkononi! 
Inanikera sana yani, natamani wangekua wanasema mapema ili nigeuze 
palepale Airport, lakini wajanja hawakuambii!!”
Swali jingine likawa linahusu njia anayoitumia kusafiri safari za mbali, DJ Khaled alisema >>“….mimi
 kusafiri natumia basi na nimenunua private bus yangu kurahisisha kazi, 
yani hata iwe safari ya wapi nitakuja na basi, hata kuja hapa Los Angeles
 kwa ajili ya hii interview nimekuja na basi, hapa nlipo nina miaka 6 
ama 7 sijapanda ndege na wala sina mpango wa kubadilisha msimamo huu”.
Kuhusiana na show za Kimataifa je??>>>“nipo
 kwenye mpango ambao bado unaendelea wa kununua boti yangu.. yes nipo 
kwenye mpango wa kufanya hicho kitu kwa sababu niko serious kabisa 
sitaki kupanda ndege… hata kama ikitokea basi itokee tuu ila 
asinishawishi mtu kitu chochote kuhusu kupanda ndege…sipendi na 
ninaogopa!“
No comments:
Post a Comment