Safari ya ndege ikaahirishwa kwa zaidi ya saa mbili, ishu ni nyuki waliovamia kwenye engine !!
Nyuki waliwahi kuibua stoty kubwa baada ya kuvamia ndege aina ya Boeing 757 mwaka 1996 ambapo
 ndani ya dakika tano baada ya kuondoka ilikuwa ishu baada ya 
kugundulika kwamba sehemu ambayo inaonesha mwendokasi wa ndege imezibwa 
na kundi la nyuki.
Leo 
kuna hii stori kutoka Uingereza inayohusisha nyuki na ndege.. abiria 
walilazimika kukaa kwa masaa mawili baada ya nyuki kuingia kwenye moja 
ya mitambo ya injini za ndege, haikuwa salama sana ndege hiyo kuanza 
safari wakati kuna hali hiyo.
Ndege hiyo inayoitwa Flybe yenye namba BE384 ilikuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin.
Shirika linalomiliki ndege hiyo limesema
 isingekuwa salama sana wao kuendelea na safari wakati nyuki wako ndani 
ya injini, ilibidi watolewe na baadae safari yao ikaendelea..

No comments:
Post a Comment