Tofauti ndani ya Real Madrid.
Zikiwa zimepita siku tano pekee tangu Rafael Benitez alipotambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid kufuatia klabu hiyo kumfukuza kazi Mtaliano Carlo Ancelotti , tayari kocha huyu mpya ameanza kutunishiana misuli na uongozi wa klabu hii ya kifalme yenye maskani yake katikati ya mji mkuu wa Hispania .
Rafa Benitez kwa mujibu wa ripoti zilizoibuka hii leo ametofautiana maoni na bosi wake ambaye ni rais wa klabu hiyo Florentino Perez juu ya mshambuliaji atayaesajiliwa na klabu hiyo ili kuimairisha kikosi chake cha msimu wa mwaka 2015/2016.
Gazeti moja la kila siku nchini Hispania la habari za michezo limeripoti kuwa Rafael Benitez anataka kumrudisha mshambuliaji aliyeuzwa toka Madrid Alvaro Morata baada ya kuridhishwa na kiwango alichokionyesha msimu huu .
Matamanaio haya ya Benitez kumsajili Alvaro Moratta yanakwenda kinyume na Perez ambaye anataka kumsajili Sergio Aguerro ili aweze kuiongoza safu ya mashambulizi ya Real Madrid kwa ajili ya msimu ujao .
Perez amekuwa na utamaduni wa kusajili wachezaji nyota wenye majina makubwa kwa karibu kila msimu ili kuifanya klabu hiyo itengeneze fedha kutokana na biashara inayofanyika nje ya uwanja .
Hata hivyo bado haijafahamika kama tofauti hii inaweza kuwa na athari yoyote kwenye ufanyaji kazi wa Rafa Benitez lakini itakuwa ishara ya kwanza ya aina ya mazingira ambayo anatajia kuyakuta akiwa ameanza kazi rasmi kama kocha wa moja kati ya klabu kubwa kuliko zote duniani
No comments:
Post a Comment