Balozi Liberata Mulamula akabidhiwa rasmi Ofisi
 Katibu 
Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi
 Liberata Mulamula akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa 
Wizara hiyo  Balozi John Haule. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mulamula 
alikuwa Balozi  wa Tanzania nchini Marekani na Mhe.  Haule kwa sasa ni 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani 
leo tarehe 01 Juni, 2015.(P.T)
 Katibu 
Mkuu, Balozi Mulamula akiwa kwenye Mkutano na baadhi ya Wakurugenzi na 
Wakuu wa Vitengo mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Balozi Haule.
 Mkurugenzi
 wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi 
(wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. 
Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango
 Bw. James Lugaganya na  Balozi Haule wakimsikiliza Balozi Mulamula 
 (hayupo pichani)
Balozi 
Mulamula akizungumza huku Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na 
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya, (kulia kwa Balozi 
Mulamula), Mhasibu Mkuu Bw. Paul Kabale (wa tatu kutoka kushoto), 
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mambo ya Nje, Bw. Mathias Abisai na Afisa 
Habari wa Mambo ya Nje Bw. Ally Kondo.Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment