Yemen: video ya mateka wa Ufaransa yarushwa hewani
Maandamano ya kuomba kuachiliwa huru kwa Isabelle Prime, Sanaa, Machi 9 mwaka 2015.
Na RFI
Video
ambayo ameonekana mateka wa Ufaransa Isabelle Prime imerushwa hewani
Jumatatu wiki hii. Isabelle Prime alitekwa nyara Februari 24 mwaka huu
katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Video
hiyo imethibitishwa na wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, ambayo
imehakikisha kwamba idara zote za serikali " zimesimama kidete "
kuhakikisha kuwa mateka huyo anachiliwa huru.
Katika
video hiyo ya sekunde ishirini na moja, Isabelle Prime ameonekana
akivalia nguo nyeusi, huku akiikaa sakafuni, na akiwaomba marais wa
Ufaransa François Hollande na wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi, msaada
ili aweze kuachiliwa huru. "Tafadhali mnisafirishe Ufarnsa haraka
iwezekanavyo ”, amesema mateka huyo.
“ Hii ni
video ambamo ameonekana Isabelle Prime ”, naibu msemaji wa wizara ya
mambo ya nje ya Ufaransa Alexandre Giorgini amesema, akithibitisha
uhalali wa video hiyo, ambayo Rfi hakipendelea kuirusha hewani kwenye
tovuti yake.
“ Idara
zote za serikali ambazo zina uwezo zimesimama kwa pamoja ili kuhakikisha
kuwa raia huyo wa Ufaransa na mkalimani wake wanaachiliwa huru “,
amesema Alexandre Giorgini,
Rais wa
Ufaransa aliomba kuachiliwa huru kwa mateka huyo baada ya kutekwa nyara
Februari 24 katika mji wa Sanaa. Ni kwa mara ya kwanza picha za mateka
huyo zinawekwa hadharani tangu kutekwa kwake nyara.
Isabelle
Prime mwenye umri wa miaka 30, alitekwa nyara akijielekeza kazini kwake,
akiwa ameambatana na mkalimani wake Chérine Makkaoui. Watu waliohusika
na kisa hicho walikua walijificha nyuso zao
No comments:
Post a Comment