Serena atinga fainali French Open 2015

Serena William,mchezaji tenis nambari moja duniani akifurahia ushindi.
Serena 
Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French 
Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na 
kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu 
kucheza fainali za mwaka huu.
Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi.
Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.
        
Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa.
Mapema 
katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa 
nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika 
fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi 
cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii.(Muro)
No comments:
Post a Comment