Idadi ya waliofariki Ghana yafikia 175

Ghana moto

Ghana moto

Moto Ghana

Takriban 
watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo 
kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo 
uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo 
walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha 
raia wengi bila makaazi pamoja na stima.
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra.
Tarayi Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Mlipuko 
huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi 
katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio.CHANZO:HABARI LEO(Muro)
No comments:
Post a Comment